Sunday, July 19, 2015

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM JOHN POMBE MAGUFULI AKITAMBULISHA KWAO

 Mbunge wa Chato na Mgombea Urais kwa chama cha Mapinduzi
CCM,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa mji huo waliojitokeza kwa wingi kumlaki,mara baada ya kuwasili leo jioni mjini humo akitokea mkoani Mwanza ambako nako alipita kujitambulisha na kuwashukuru wakazi wa jiji hilo ambao nao walijitokeza kwa wingi.
Kufuatia ujio wa Dkt Magufuli ndani ya mji wa Chato kuliibuka shamra shamra za mapokezi zilizokuwa zikirindima kila pande wakifurahia uteuzi wa
CCM kwa Dkt Magufuli.


 Baadhi ya Wananchi wa Wilaya ya Chato na vitongoji vyake waliokuwa
wamekusanyika kwenye kituo cha mabasi wilayani humo wakishangilia kwa
furaha kubwa mara baada ya Mbunge wao na Mgombea Urais kwa chama cha
Mapinduzi  CCM,Dkt John Pombe Magufuli kujitambulisha kwao.

No comments:

Post a Comment