Wednesday, July 15, 2015

KADA WA CCM MWALIMU RUBEIYUKA ALIYETANGAZA KUCHUANA NA BALOZI KAGASHEKI WENYE KITI CHA UBUNGE JIMBO LA BUKOBA MJINI ACHUKUA FOMU


Katibu wa uchumi na fedha wa Bukoba mjini, Mwalimu George Rubeiuyuka aliyetangaza mapema nia yake ya kuwania kiti cha ubunge katika  jimbo la Bukoba mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jana (jumatano) amekuwa kada wa kwanza kuchukua fomu ya kwania kiti cha ubunge wa jimbo hilo.


Mwalimu George ambaye nia afisa elimu vifaa na takwimu wa wilaya ya Misenyi amechukua fomu hiyo majira ya saa 4.30 toka kwa katibu msaidizi wa Bukoba mjini Abdul Kambuga huku akiwa ameongozana na wafuasi wachache wa chama hicho.


Kada huyo wa CCM muda mfupi baada ya kuchukua fomu hiyo  alisikika akisema kuwa hakuwania nafasi hiyo ya ubunge wa jimbo la Bukoba mjini inayoshikiliwa na Balozi Khamis Kagasheki  inayonyemelewa na  makada wengine wa chama hicho kwa ushabiki.


Amesema anawania nafasi hiyo kwa dhati kwa kuwa uzoefu wa kuwaongoza wananchi  anao, uwezo wa kuwatumikia anao, uwezo wa kukitetea chama anao na sababu nia na madhumuni ya kuwania nafasi ya ubunge katika jimbo la Bukoba mjini anayo.


Mwalimu Rubeiyuka amesema kwa sasa ni mapema kutaja vipaumbele vyake kwa kuwa  vipaumbele vyake vitaendana sambamba na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 205 itayotolewa na chama hicho.


Allichokiahidi ni kuwatumikia wananchi kwa nguvu zote, pia amesema kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha anaondoa makundi yanayodumaza maendeleo katika manispaa ya Bukoba, amesema makundi ndio chanzo cha migogoro inayokwamisha maendeleo katika manispaa ya Bukoba.


Amewaomba wanachama wa CCM wammchague ili aweze kupeperusha bendera ya chama hicho kikongwe nchini  kwa kuwa anao uwezo mkubwa wa kukabiliana na wawakilishi wa vyama vya watakaoteuliwa kuwania nafasi ya ubunge ndani katika jimbo la Bukoba mjini.


Kinyanganyiro cha kumpata mwakilishi atakayepeperusha bendera ya CCM katika jimbo la Bukoba mjini kina ushindani mkubwa, ushindani huo unadhihirishwa na hatua ya  makada wengi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo.


Baadhi ya makada ambao wanatarajia kuchukua fomu kwa lengo la kushiriki kwenye kura za maoni za CCM ni pamoja na Meya wa zamani Anatory Amani ambaye ni hasimu mkubwa wa mbunge wa sasa Balozi Kagasheki, Samweli Rugemalila na Joseph Mujuni Kataraiya hali hii tofauti na vipindi vilivyopita ambapo Balozi Kagasheki alikuwa akipita bila kupingwa.

No comments:

Post a Comment