Thursday, June 04, 2015

Taarifa wafanyakazi Marekani zadakuliwa

Serikali ya marekani yakumbwa na udukuzi mtandao wa komputa ambapo taarifa binafsi za mamilioini ya wafanyakazi wa serikali zimeingiliwa.
Ofisi ya Utumishi ya nchini hiyo inasema karibu ya watu milioni nne ambao wanafanya kazi au waliwahi kufanya kazi wameathirika na udakuzi huo.
Idara ya Utumishi ya Serikali ya Marekani inayosimamisha huduma za wafanyakazi wa umma nchini huo imefanya uchunguzi wa usalama wa taarifa za wafanyakazi wake wapatao milioni nne.
Idara hiyo inasema wadakuzi hao walililenga kuingilia taarifa hizo kwa njia ya mtandao tangu mwezi aprili jambo linalofanyiwa uchunguzi na shirika la kijasusi la FBI.
Taarifa zote za udakuzi huo na idadi ya watu waliohusika bado haijafahamika lakini Afisa mmoja anasema kila idara ya serikali itakuwa imeathirika kwa kiasi kikubwa.
Mjumbe wa Kamati ya kiintelejensia ya Baraza la Seneti imewalamu wadakuzi kutoka nchini China kuhusika na udakuzi huo.
Hii sio mara ya kwanza kwa taarifa muhimu kama kama hizo kufanyiwa udakuzi.
Mwezi Machi mwaka jana,wadakuzi walijaribu kufanya udakuzi kwa wafanyakazi wa serikalini ambapo pia mwezi Novemba taarifa za za wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya ndani wapatao elfu ishirini zilidakuliwa.

No comments:

Post a Comment