Tuesday, March 03, 2015

WATANZANIA WASHAURI KUZIPUUZA KAULI ZA ZINAZOENEZWA ZENYE LENGO LA KUIKWAMISHA KATIBA


NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA, TANZANIA +255 784 939586/ 753 844 995
 
Watanzania wameshauriwa kuzipuuza kauli za ushawishi  zinazotolewa na na baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa  zenye lengo la kuikwamisha  rasimu ya katiba ya jamhuri ya muungano iliyopendeklezwa kwa maslahi ya vyama vyao vya siasa  badala yake  waisome kwa umakni zaidi katiba hiyo ili waipigie kura kulingana na namna walivyoielewa.
 
Ushauri huo umetolewa na baadhi ya wadau mbalimbali ambao ni pamoja na viongozi wa madhehebu ya dihi, vyama vya siasa, mashirika yasiyo ya kiserikali na  asazi za kiraia wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa zoezi la usambazaji wa katiba kwa wananchi uliofanywa  na halmashauri ya manispaa ya BUKOBA.
 
Wamesema  wale wanaojaribu kuwashawishi wananchi waipigie kura ya hapana katiba iliyopendekezwa  kwamba hawana nia njema na nchi hii, waliahidi kutumia nafasi zao walizonazo kuwahamasisha wanachi waisome katiba  ili wachukue uamzi ulio sahihi wakati  muda kuipigia kura ukifika  kama wanavyoeleza.
 

 
Lengo la kusambaza  rasimu ya katika iliyopendekezwa kwa wananchi ni kuhakikisha wananchi wanapata fiursa  ya kuisoma na kuielewa kabla ya kuipigia kura .
 

No comments:

Post a Comment