Thursday, March 19, 2015

WANANCHI KATIKA KATA YA KITENDAGULO WATAKIWA KUWAFICHUA WANAOWAHISI WANAJIHUSISHA NAVITENDO VYA MAUAJI


NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA

Kufuatia  matukio  yanayofanywa na watu wasiojulikana katika kata ya KITENDAGULO iliyoko  manispaa ya BUKOBA  ya kuwauna watu kwa kuwakata kata na mapanga yanayohusishwa na imani za kishirikina, serikali imewaomba wananchi kuwafichua wale wote wanaowahisi wanaojihusisha na matukio hayo badala ya kuwaonea aibu ili waendelee kuishi kwa amani na kwa usalama zaidi.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya BUKOBA, JACKON MSOME ambaye amekutana na  na wananchi wa mtaa ya KAGEMU ulioko katika kata ya KITENDAGULO kwa lengo la kuwapa pole ndugu na jamaa wa marehemu WAWILI waliouwawa kwa siku moja katika kata hiyo kwa kukatwa katwa na mapanga.

MSOME amewaambia wananchi kuwafichua wale wote wanawatilia mashaka kwa kutoa taarifa juu yao  kwa kiongozi yoyote  bila bla kuwaonea aibu na bila kujali nafasi yao wallizonazo ndani ya jamii ili serikali iweze kuwachukulia hatua za kisheria.



Kwa upande wake,Mkuu wa kituo cha polisi cha kati Bukoba, FRANK UTONGO amewahakikishia wananchi kuwa jeshi hilo litafanya doria endelevu katika kata hiyo,   nao baadhi ya wananchi katika kata hiyo ambao n FRANCIS  RWEGASIRA na DEOGRATIAS RUSIZOKA ni miongoni mwa wananchi katika mkoa wa KAGERA wanaotoa ushauri wa namna ya kudhibiti vitendo hivyo.



Kata ya KITENGAGURO ni kata ziliko mkoani KAGERA ambayo imekubwa na wimbi la mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana, mauaji katika kata hiyo yalianza tangu mwishoni mwa mwaka jana, hadi sasa zaidi ya watu NANE wameishauwawa.




No comments:

Post a Comment