Monday, March 09, 2015

RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NJOMBE – HALMASHAURI YA MJI WA NJOMBE

NEMBO Govt

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI

RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU NJOMBE – HALMASHAURI YA  MJI WA NJOMBE

nembo%20ya%20NEC

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

MKOANI NJOMBE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura  kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa.
 Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
·        Waliotimiza umri wa Miaka 18 na  kuendelea  na wale wote  watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·        Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·        Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha  lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari.
Zoezi litaanza kufanyika Wilayani Njombe katika Halmashauri ya Mji Mdogo wa Makambako.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako  kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka  tarehe 01/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Kumbuka:-
Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.

       Tangazo hili limetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, S.L.P. 10923, Dar es Salaam

UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA

MKOANI NJOMBE

Tume ya Taifa ya Uchaguzi inawatangazia wananchi wote wa Mkoa wa Njombe,Halmashauri ya Mji mdogo wa Makambako kuwa itaanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa kutumia teknolojia ya “Biometric Voters Registration” kuanzia tarehe 23/02/2015 hadi tarehe 01/03/2015 katika kata ya Kitisi, Kivavi, Lyamkena, Maguvani, Majengo, Makambako, Mjimwema, Mlowa, na Mwembetogwa. Kata ya Kitandililo utafanyika tarehe 03 -09/03/2015. Kata ya Mahongole tarehe 11-17/03/2015 na Kata ya Utengule uboreshaji utafanyika tarehe 19 – 25/03/2015.
Vituo vya Uandikishaji vitakuwa kwenye Vijiji, Vitongoji na Mitaa
 Watakaohusika katika zoezi hili ni wananchi wote:-
·        Waliotimiza umri wa Miaka 18 na  kuendelea  na wale wote  watakaotimiza miaka 18 ifikapo mwezi Oktoba, 2015.
·        Waliojiandikisha awali kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura la zamani ili kuhuisha taarifa zao na kupata kadi mpya za kupigia kura.
·        Wale wote ambao wanazo sifa za kujiandikisha  lakini hawajawahi kujiandikisha kwenye Daftari
Zoezi litaanza kufanyika Mkoani Njombe katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na Mji wa Njombe.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi inasisitiza wananchi wote wa Mji Mdogo wa Makambako  kujitokeza kwa wingi kuanzia tarehe 23/2/2015 mpaka  tarehe 25/03/2015 kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuwawezesha kupiga Kura ya Maoni na kuchagua Viongozi wao katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu 2015.
Vituo vya kujiandikisha vitafunguliwa kuanzia saa 2:00 Asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni
Kumbuka:-
Hutaweza kupiga Kura ya Maoni au Kupiga Kura wakati wa Uchaguzi Mkuu kama utakuwa hujajiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Nenda kajiandikishe sasa.

Ruth Masham

No comments:

Post a Comment