Tuesday, February 17, 2015

WALIOFANYA UBADHILIFU WA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA MANISPAA YA BUKOBA KUKIONA CHA MOTO




 
NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na serikali kimeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu viongozi wa kuchaguliwa na wananchi waliopewa jukumu la kusimamia   halmashauri ya manispaa ya BUKOBA  na baadhi ya watumishi waliofanya  ubadhilifu wa  fedha  zilizokuwa zimetengwa  kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa katika manispaa hiyo .
 
Kauli hiyo imetolewa na NAPE NNAUYE,  katibu wa siasa itikadi na uenezi wa  taifa wa Chama Cha Mapinduzi CCM  kwenye hotuba yake aliyoitoa  kwenye maalumu mkutano wa hadhara ulifanyika kwenye uwanja wa uhuru wa kumsimika  DEONIZ MALINZI aliyeteuliwa kuwa kamanda wa jumuia ya  vijana  katika  mkoa wa KAGERA.
 
Sambamba na kauli hiyo, katibu huyo amemuagiza mkuu wa mkoa wa KAGERA , JOHN MONGELLA kuhakikisha anatafuta ufumbuzi  migogoro iliyochangia kukwamisha  miradi ya maendeleo katika manispaa hiyo iliyochangiwa na hatua ya baadhi ya  madiwani kugomea vikao vya baraza kwa zaidi ya miaka MIWILI jambo  lililodumaza maendeleo ya wananchi.
 

 
Katika mkutano huo Balozi KHAMIS KAGASHEKI  mbunge wa jimbo la BUKOBA mjini amenusha kwamba yeye sio chanzo cha migogoro iliyokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo  katika manispaa hiyo bali yeye ni mtetezi wa wananchi, nao makada wa CCM,  AMIM  AHMED na PROTACE ISHENGOMA wanaeleza  namna chama hicho kilivyojipanga kuwawezesha vijana  kiuchumi huku wakiwahimiza  vijana kujiunga na vyama vya akiba na mikopo.
 

 
SADIK HASSAN ni mwenyekiti wa VIjana wa CCM wilaya ya NGARA anayewaleza vijana wajiepushe na udanganyifu unaofanywa na viongozi wa vyama vya upinzani  na kuwataka pia wasikubali kurubuniwa,  huku DIONIZ MALINZI kamanda wa vijana wa mkoa wa KAGERA akiahidi kuiimarisha jumuia ya vijana katika mkoa huo.
 

 
Mgogoro katika manispaa ya BUKOBA ulikwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa soko kuu la BUKOBA, upimaji wa viwanja ELFU tano, ujenzi wa standi kuu ya mabasi eneo la KYAKAILABWA na jingo la kitega uchumi.
 
Baadhi ya viongozi ambao ni madiwani wakiongozwa na BALOZI KAGASHEKI walipinga utekelezwaji wa miradi hiyo kwa madai kuwa ilikuwa imeghubikwa na vitendo vya ubadhilifu hali ambayo iliwagawa madiwani hadi baadhi yao wakafikia hatua ya kususia bikao.


No comments:

Post a Comment