Tuesday, February 10, 2015

MKOA WA KAGERA WAJIZATITI KUTHIBITI VIFO VYA WAKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO

www.bukobawadau.blogspot.comwww.issamichuzi.blogspot.com


NA AUDAX MUTIGANZI

BUKOBA


Kamati ya huduma ya afya ya msingi  katika mkoa wa KAGERA imefanya kikao cha dharura kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali yenye lengo la kupunguza  vifo vya watoto wachanga chini ya umri wa miaka MITANO na wakina mama wajawazito.


Kikao hicho kimefanyika wilayani KARAGWE  kwenye ukumbi wa  hoteli ya kanisa la kiinjili la KIRUTHERI  diosisi ya KARAGWE iliyoko katika mji wa mdogo  wa KAYANGA chini ya mkuu wa mkoa wa  KAGERA, JOHN MONGELLA.


Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na  viongozi mbalimbali wa serikali katika ngazi zote, mkuu huyo wa mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya mkoa humo  katika kila vikao wanavyoviandaa  vya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo kuweka ajenda ya namna ya kudhibiti vya vifo vya watoto wachanga chini ya miaka MITANO na  wakina mama wajawazito.





DKT THOMAS RUTACHUNZIBWA ni mganga mkuu wa mkoa wa KAGERA na NEEMA KYAMBA mratibu wa huduma ya watoto na wakina mama wajawazito  katika mkoa huo ni maofisa wa afya wanaoeleza  hali ya sasa ya  vifo vya watoto na wakina mama.




 Kwa upande wake GRANDIOSA TIBAIJUKA  ambaye ni meneja taaluma wa mradi wa JHPIEGO unaofadhiliwa na seriikali ya MAREKANI  anaishauri jamii kuchangia huduma ya afya ili iweze kupata matibabu sahihi badala ya kutegemea sana misaada toka kwa serikalini  na wafadhili, DALI  RWEGASIRA mkuu wa wilaya ya KARAGWE na DENIS MBEO mkuu wa wa wilaya ya BIHARAMULO ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wanaoeleza mikakati yao ya  namna ya kuthibiti vifo vya wakina mama na watoto kwa kuwahamasisha  wananchi wajiunge na mfuko wa afya ya jamii.




Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache hapa nchini ambazo inafanya mikakati mikubwa ya kuhakikisha vifo vya wakina mama wajawazito na watoto cinini ya miaka MITANO vinabaki kwenye vitabu vya historia, mkakati wa mkoa huo ni kuihamasisha jamii namna ya kujiepusha na vifo hivyo kuanzia ngazi ya vijiji, mtaa na vitongoji.

No comments:

Post a Comment