Tuesday, February 10, 2015

MAHAKAMA YA RUFANI NCHINI KUSIKILIZA MASHAURI ISHIRINI NA SITA KAGERA


NA MHARIRI
AUDAX MUTIGANZI +255 784 939 586/ 753 844 995





Mahakama kuu kanda ya BUKOBA imezindua kikao vya mahakama ya rufaa ambapo mashauri mbalimbali ISHIRINI na SITA   yatasikilizwa huku  mengine yakitolewa  maamuz na jopo la majaji wa mahakama hiyo, uzinduzi wa vikao hivyo umefanyika leo  kwenye viwanja vya mahakama hiyo iliyoko katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.



Uzinduzi huo   ulienda sambamba  na gwaride maalumu lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la polisi cha kutuliza ghasia lililokaguliwa  na jaji EDWARD RUTAKANGWA ambaye ni mwenyekiti wa  majaji watakaosikiliza mashauri yote yatakayoletwa  mbele ya mahakama ya rufaa uliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali walioongozwa na mkuu wa mkoa wa KAGERA JOHN MONGELLA..



Akitoa  wakati wa uzinduzi huo ,CHARLES MAGESSA ambaye  msajili wa mahakama kuu kanda ya BUKOBA amesema  sambamba na kikao vya mahakama hiyo ya rufani pia mahakama  kuu kanda ya BUKOBA itakuwa  kikao kitakachoanza leo  katika vituo viwili ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na BUKOBA na BIHARAMULO ambapo  jumla ua mashauri ISHIRINI na SABA yatasikilizwa.





Aidha , msajili huyo  amesema mahakama hiyo imeandaa vikao hivyo kwa washirikisha wadau wakuu wa mahakama hiyo ambao aliwataja kuwa ni pamoja na jeshi la polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, MAGESSA amesema  asilimia kubwa ya  wakaotoa ushahidi unaohusiana na mashauri yatakayosikilizwa kwamba wanaonyesha mwitikioa mzuri.





Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhulia uzinduzi wa vikao hivyo wameshukuru hatua ya serikali ya kusogeza huduma mahakama ya rufani katika mkoa wa KAGERA, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa uwepo wa Mahakama ya rufani katika mkoa wa KAGERA utawapa nafasi kubwa ya kutetea haki zao ambazo wakati mwingine walikuwa wakipokonywa walikuwa wakifuiata huduma ya mahakama ya rufani mkoani MWANZA.

Kabla  ya serikali kusogeza huduma ya  mahakama ya rufani mkoani KAGERA mwaka jana, wananchi walikuwa wakisafiri hadi mkoani  MWANZA kusikiliza mashauri yao, hali hiyo ilikuwa ikiwapa wakati mgumu  wananchi hao  hasa wenye kipato kidogo wakatii mwingine walikuwa wakilazimika kupoteza haki yao, wengi walikuwa wakishindwa kumudu gharama za usafiri na malazi.


No comments:

Post a Comment