Tuesday, February 10, 2015

DR KAMALA ATEMBELEA MAONYESHO YA UTALII BRUSELS

 Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimshukuru mwakilishi wa kampuni ya utalii ya Escape Bwana Nassri Chaouki baada ya kutembelea banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala aliishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania.

 Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P AKIWA katika picha ya pamoja na Bwana Burt Munting Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Habari Travel ya Uganda inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Masoko wa kampuni ya kutangaza utalii ya Travel Xenarjo ya Ubeligiji Bi. Dana Maes baada ya kutembelea Banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Kampuni hiyo imekubali kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania baada ya Balozi Kamala kuiomba kampuni hiyo kufanya hivyo.

No comments:

Post a Comment