Wednesday, March 19, 2014

UKWELI MCHUNGU: WAPINZANI HAWANA SIFA ZA KUONGOZA NCHI. (A COMPARATIVE ANALYSIS)


Siasa ama chama chochote cha siasa ni zao la falsafa. Kuwa Mwanasiasa bila kuwa na falsafa ama kuwa na Chama cha Siasa ambacho hakina msingi wa falsafa ni kasoro kubwa ambayo hufanya mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutofanikiwa katika lengo lake kuu. Kukosa falsafa kunasababisha Mwanasiasa ama Chama Cha Siasa kutokuwa na dira ya kuifuata na matokeo yake ni kufanya siasa inayoegemea katika matukio na kukosoa mawazo na mipango ya wengine ama vyama vingine bila kuwa na WAZO kuu ambalo unalisimamia kama mwanasiasa ama Chama Cha Siasa. Kila mwanadamu kwa asili ya Uanadamu wake hujengwa na imani juu ya kitu fulani, uamini katika mlengwa fulani unaofahamika kwa jina la ITIKADI, Hivyo Chama Cha Siasa ni mkusanyiko wa kundi la watu ambao wanaamini katika ITIKADI moja, hivyo tukiitaja CCM directly tunataja UJAMAA kama ITIKADI kuu ambayo wanachama na Viongozi wa CCM wanaiamini na kuitetea kwa hoja na nguvu zote. 

Utangulizi huo unamaana moja kuu katika makala hii niliyoipa jina "UKWELI MCHUNGU" kuwa CCM imejipambanua kwa itikadi yake na kuisimamia popote pale, wapinzani hawana msingi unaotokana na ITIKADI na SERA, wamejikita katika kufanya siasa za matukio na UBISHANI. Siasa isiyo endelevu kwani matukio hukoma kwa wakati fulani, hivyo kwa wananchi walio makini hawawezi kuamini katika Chama ambacho chenyewe hakina kitu ama falsafa inayoiamini. Wananchi wanahitaji viongozi wenye falsafa wanayoiamini.

Katiba ya nchi yetu iko wazi kuwa sera kuu ni Ujamaa na Kujitegemea, vyama vya siasa vilipaswa kujipambanua kisera kuona nani zaidi katika kufikia sera hiyo kuu. CCM inajimbanua vyema katika hili, kuwa na vyama vya siasa vinavyoamini nje ya itikadi hiyo ya Taifa ni kuvunja Katiba lakini msingi wake ni kutowajibika sawasawa kwani hili lilipaswa kuangaliwa kuanzia kwenye hatua ya usajili wa Vyama. Matokeo yake ni kuja kuwa Chama ambacho kitaongoza nchi nje ya mifumo yake ya kikatiba na hivyo kuzaa uongozi dhaifu, usiozingatia na hata kuvunja katiba ya nchi.

Maana ya kuwa na Vyama vya upinzani ni kutaka kuwapa wananchi alternative ya Uongozi na falsafa. sio KAZI ya upinzani kupinga kila kitu na sio kazi ya upinzani kusifia serikali, kimsingi kazi ya upinzani ni kutoa the best alternative solution to justify that opposition is the best alternative government in waiting. Lazima upinzani ujijenge kisera, kifalsafa na kiitikadi ambayo wananchi wataona kuwa ni njia ya kufikia Maendeleo na kuwajengea matumaini ya Mafanikio na Maisha Bora (kwani ndio paramount demand ya wananchi - MAISHA BORA)


Na nasema kama Upinzani ungekuwa makini basi Serikali na Chama Kilicho Madarakani nikimaanisha Chama Changu CCM kingekuwa makini zaidi, MWALIMU Nyerere aliwahi kusema maneno ambayo mpaka leo yamewekwa kwenye bango mbele ya Ukumbi wa Mikutano ya NEC (maarufu kama whitehouse) pale Makao makuu dodoma, maneno yale yanasema " Bila CCM madhubuti nchi yetu itayumba, na Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM "


TANZANIA imekosa UPINZANI MAKINI, upinzani unaojitambua nini unataka na wafanye nini kufikia hicho wanachokitaka. Wachambuzi wa siasa wanapoangalia uimara wa upinzani moja ya kigezo ni kutathimini uwezo wa mawaziri (Viongozi) na watendaji wa Chama tawala na Serikalini yake ukilinganisha na mawaziri Vivuli,na viongozi wa Upinzani. Inatakiwa Shadow Cabinet ioneshe uwezo na matumaini kuliko cabinet. Upinzani uoneshe matumaini na uwezo kuliko CCM. 


Wananchi wanaangalia alternative ambayo wapinzani wanakuja nayo, wanafanya comparison analysis ya viongozi hao yaani kwa mfano, kwenye baraza la mawaziri na mawaziri vivuli:
wananchi wanaangalia kambi ya upinzani bungeni kama mfano wa Uwezo wa Viongozi wa Upinzaniti, wanaangalia kati ya:


·         Lema V/s Chikawe kwenye Wizara ya mambo ya ndani, wanajiuliza hivi ni kweli LEMA anaweza kuwa best alternative ya CHIKAWE.., kweli..?
·         Selasini V/s Dr Mwinyi kwenye Wizara ya Ulinzi, wananchi wanawapima kwa uwezo wao.

·         SUGU v/s Dr Mukangara kwenye wizara ya habari, utamaduni na michezo, wananchi wanajiuliza hivi ni kweli SUGU anaweza kuwa bora mbele ya Dr Mukangara hata washawishike kukiondoa Chama kilichomsimamisha Dr Mukangara wakipe Chama kilichowaletea SUGU kama best alternative..., kweli..?

·         Msigwa v/s Lazaro Nyalandu kwenye wizara ya Maliasili.

Wenye v/s Bernard Kamilius Membe kwenye Wizara ya Mambo ya nje.,wananchi wanajiuliza hivi kweli MEMBE akisimama na WENJE..,Wenje anaweza kuonekana bora na kiongozi wa maana mbele ya MEMBE..? wananchi makini wanayaona haya na kuyapima na kisha kufanya uamuzi kupitia sanduku la KURA.

Kwa tathimini hiyo fupi, na hata kwa Uongozi wa juu wa Vyama vya upinzani., mathalani Chama kikuu cha Upinzani yaani Chadema.,ukifanya tathimini kwa Umakini juu ya Aina na Uwezo wa Viongozi wake dhidi ya wale wa Chama Makini CCM, wananchi wanaona matumaini na future bora ya nchi kupitia CCM.

Mathalani tazama mifano hii:

·         Wenyeviti; CHADEMA-MBOWE dhidi ya CCM-KIKWETE
·         Makamu M/kiti: CHADEMA-resigned ARFI dhidi ya CCM-MANGULA
·         Katibu Mkuu: CHADEMA - DR. SLAA dhidi ya CCM- KINANA
·         Naibu K/mkuu: CHADEMA - suspended ZITTO dhidi ya CCM- MWIGULU


Ukiangalia kwa Upande wa Sekretaieti ya CCM

1.     NAPE NNAUYE
2.     MAMA ASHA-ROSE MIGIRO
3.     MAMA ZAKHIA MEGHJI
4.     DR SEIF KHATIBU


Kwa upande wa CHADEMA.

1.     ANTHONY KOMU
2.     JOHN MNYIKA
3.     LEMA GODBLESS
4.     TUNDU LISSU
5.     LWAKATARE
6.     BENSONI KIGAILA
7.     JOHN MREMA


Wananchi makini wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wanawapima viongozi wao kwa kutathimini uwezo, maarifa, na uzoefu. kwa tathimini hii ni Vipi watanzania wanaweza kuwapa Upinzani nchi hii., kwa tathmini hii ni wazi CCM itaendelea kuwa Chama bora na kitakachoendelea kutawala nchi hii kwa miaka mingine hamsini na dahari.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Vivaa Vijana Vivaaa.

VIJANA KARIBUNI CCM na kazi iendelee.

No comments:

Post a Comment