Monday, March 31, 2014

PINDA AKABIDHI TUZO YA MWANAMKE BORA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika hafla  ya kutoa tuzo ya Global Publishers iliyotolewa kwa mwanamke bora nchini mjini Dodoma Machi 29, 2014. Wengine pichani  kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigogo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Lephy Gembe na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Pindi Chana. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2014 ya Global Publishers, Profesa Anna Tibaijuka  mjini Dodoma machi 29, 2014. Katikati ni Mkurugenzi wa Global Publishers, Eric Shigongo. (Picha na Ofisi ya  Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa Tuzo ya Mwanamke Bora wa Mwaka 2014 ya Global Publishers baada ya kuwatunuku tuzo zao mjini Dodoma Machi 29, 2014.  Kutoka kushoto ni Anna Abdallah ambaye alipokea kwaniaba ya Dr. Asha Rose Migiro, Anne Kilango, Maria Kham na Profesa Anna Tibaijuka. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment