Monday, March 24, 2014

MAMBO YA KAMPENI YA UBUNGE JIMBO LA CHALINZE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwa amemuinua mkono Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete ikiwa ni ishara ya kumnadi kwa wananchi wa Kata ya Ubena Zomozi huku mvua kubwa ikiendelea kunyesha,wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea katika Kata mbali mbali ndani ya jimbo la Chalinze.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi na wanaCCM wa Kata ya Ubena Zomozi huku akishangilia kwa shangwe,leo Machi 24,2014.
 Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwapungua mkono wananchi na wapenzi wa CCM katika Kata ya Ubena Zomozi,leo Machi 24, 2014.Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Ndg. Abdulrahman Kinana.

No comments:

Post a Comment