Sunday, February 09, 2014

KAMPUNI YA UTALII YA UBELGIJI YAINADI TANZANIA

  Bwana Damian George Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Utalii ya African Breakaway Safaris akinadi vivutio vya utalii vya Tanzania katika Maonesho ya Utalii yanayoendelea jijini Brussels.

  Bi. Laurence Joiris wa kampuni ya Bel Afrika ya Ubelgiji akinadi vivutio vya utalii vya Tanzania katika Maonesho ya Utalii yanayoendelea Brussels.
 Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimsikiliza mwakilishi wa kampuni ya Utalii ya Reisspeciliast ya Ubelgiji akimweleza jinsi kampuni hiyo inavyopeleka watalii  Tanzania mara mbili kwa mwaka na jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo kuitangaza Tanzania Ubelgiji. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo na ameiomba iendelee kuitangaza Tanzania.
Dr. Remo wa Ubelgiji akifurahia kahawa ya Tanzania katika banda la Tanzania la Maonesho ya Utalii yanayoendelea jijini Brussels.

No comments:

Post a Comment