Wednesday, October 02, 2013

ZIARA YA WAZIRI MKUU PINDA MKOANI KIGOMA

 Waziri Mkuu, MIzengo Pinda  akitazama  bunduki, risasi na  silaha
mbalimbali  zinazolipuka vilivyokamatwa na  Jeshi la polisi  mkoani
Kigoma kutoka kwa watu waliokuwa wakizilmiki kinyume cha sheria,
Oktoba 2, 2013. Vifaa hivyo  viko kwenye Makao Makuu ya Polisi ya mkoa
huo. Mheshimiwa Pinda yuko katika ziara ya siku sita mkoani Kigoma.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu


Naibu Waziri wa Maji, Dkt. Binilith Mahenge  (wapili kulia) akisafiri kwa boti kutoka Kigoma mjini Kwenda Kagunga . Mheshimiwa Mahenge alifuatana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye ziara ya Mkoa wa Kigoma Oktoba 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Kagunga  wilayani Kigoma vijijini wakifurahia hotuba ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakati alipohutubia Mkutano wa hadhara kijijini  hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Kigoma Oktoba 1, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

No comments:

Post a Comment