Monday, October 28, 2013



Wananchi katika manispaa ya Bukoba wanasubili kwa hamu taarifa ya timu ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) ambayo inachunguza matumizi mabaya ya madaraka inayomhusu meya wa manispaa ya Bukoba Bw. Anatory Amani.

Timu hiyo ya CAG baada ya kumaliza kazi yake ya uchunguzi inatarajia kuwasilisha taarifa hiyo kwa waziri mkuu Mizengio Pinda ambayo baadae itasomwa mbele ya kikao maalumu cha baraza la madiwani.

Taarifa hiyo ndio itatoa mwelekeo sahihi wa tuhuma zilizokuwa zinaelekezwa kwa meya huyo ambazo ziliwalazimu madiwani wakiongozwa na balozi khamis Kagasheki wafikie hatu ya kusaini waraka wa kutaka kupiga kura za maoni za kumg,oa.

Katika manispaa ya Bukoba baadhi ya madiwani wameahidi kutohudhuria vikao vitakabyoitishwa na meya huyo hadi taarifa ya CAG itakaposomwa mbele yao na kudhihirisha ukweli wa tuhuma wanazozielekeza kwa meya Amani.

Madiwani wa manispaa ya Bukoba wanadai meya anawazunguka kwa kuingia kwenye mikataba bila kuwashirisha, mikataba iliyoingiwa ambayo madiwani hao wana mashaka nayo  ni pamoja na ulw wa ujenzi wa soko jipya  la Bukoba.

Wanaitaja miradi mingine kuwa ni pamoja na upimaji wa viwanja 5,000, ujenzi wa standi kuu ya mabasi eneo la Kyabailabwa, ujenzi wa jengo la kitega uchumi standi ya mabasi ya zamani, mikopo toka TIB na miradi mingine mingi.

Madiwani hao wanadai hadi kieleweke, inaonekana hawana tena hamu na meya huyo kwa kuwa mpango wao mzima ni kutaka kumg,oa.

No comments:

Post a Comment