Thursday, August 15, 2013

NAPE, MANGULA NA MWEYEKITI WA CCM WA MKOA WA KAGERA WATOFAUTIANA

MGOGORO kati ya madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba walio kwenye harakati za kumg’oa  Mstahiki Meya wa halmashauri ya manispaa hiyo  Anatory Amani  hiyo ambao halmashauri kuu ya mkoa wa Kagera katika kikao chake ilitangaza kuwavua uanachama umeanza kuwagawa viongozi ndani ya cha hicho  kuanzia  ngazi ya mkoa ahadi  kitaifa.
 
Mgawanyiko wa viongozi hao ulianza pale  Katibu wa itifaki na uenezi wa wa chama hicho taifa, Nape Mnauye alipotoa msimamo wa chama hicho kwa kufuta  maamuzi yaliyotolewa na halmashauri hiyo kuu ya mkoa huo ya kuwavua uanachama madiwani 8 wa CCM   wanaotaka kumg’oa  Meya Amani kwa kusema kuwa hayakuwa sahihi.
 
Mnauye alitoa msimamo wa chama hicho wakati wa kikao chake na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ofisi ya chama hicho iliyoko mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam, agosti 14, mwaka huu.
 
Katika kikao hicho Nape aliwaambia waandishi wa habari kuwa kikao kilichowavua madiwani hao uanachama wa chama hicho kuwa kilikuwa sio kikao rasmi cha halmashauri kuu ya mkoa ya CCM, katika kikao hicho Mnauye alisema kuwa uamzi ulitolewa na halmashauri kuu ni batili hivyo hauwazuii kuendelea na shughili zao za kuwatumikia wananchi.
 
Katika kikao hicho Mnauye alisema kikao kitakachotoa hatima ya mgogoro kati ya Meya Amani na madiwani wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba ni kile cha halmashauri kuu ya taifa kitakachofanyika Agosti 18, mwaka huu mjini Dodoma.
 
Katika hali isiyo ya kawaida umazi ulitolewa na Mnauye wa kuwanusuru madiwani hao ulipingwa vikali na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho taifa Philip Mangula ambaye alisema kuwa anaunga mkono maamuzi yaliyotolewa na halmashauri kuu ya taifa ya kuwavua uanachama madiwani wa CCM walio kwenye harakati ya kumg’oa meya Anatory Amani.
 
Mangula alisema maamuzi yaliyotolewa na Nape yalikuwa yake binafsi na wala sio ya chama, alisema kikao kilichowavua uanachama madiwani hao kuwa kilichokuwa sahihi, kauli ambayo inapingana na iliyotolewa na Mnauye kuwa kilikuwa batili.
 
Kufuatia hali hiyo ya viongozi wa chama hicho kuchanganyana , Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Kagera Bi. Costancia Buhiye jana alikutana na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa jengo la chama hicho kuelezea maamuzi sahihi ya chama hicho.
 
Katika Kikao hicho na waandishi wa habari Bi. Buhiye alisema maamuzi yanayoheshimiwa ni yale yaliyotolewa na Makamu wa CCM taifa, Mangula na wala sio yaliyotolewa na Nape Mnauye juu ya sakata la kuwavua baadhi ya madiwani kupitia katika chama hicho uanachama.
 
Alisema maamuzi yaliyotolewa na Mnauye ni batili hivyo wananchi hasa wanachama wa CCM hawapaswi kuyasikiliza kwa kuwa yana lengo la kukigawa chama hicho, “kikao kilichogtoa maamuzi ya kuwavua uanachama madiwani kilikuwa sahihi kabisa wale wanaosema mengine wana mambo yao” alisema Bi. Buhiye kwa msisitizo.
 
Mwenyekiti huyo alisema CCM haiwezi kuendelea kuwakumbatia madiwani wanaochangia kukwamisha maendeleo, “madiwani hawa tumewavumilia sana, wakiitwa kwenye vikao hawaudhurii, kisa eti hawana imani na Meya” alisema.
 
“Ndugu nawaambia waandishi tume mbalimbali zimeundwa kuchunguza mgogoro kati ya madiwani na Meya, sasa tunasubili majibu, ziko nyingi inaonekana madiwani hawa hawana subira” alimaliza.
 
Kauli hiyi inapingwa na madiwani wanaompinga Meya, kwa nyakati tofauti walisema kuwa baadhi ya viongozi ndani ya CCM kuwa ndio wanachangia kukua kwa mgogoro kati ya Meya na Madiwani, walisema baadhi ya viongozi hao wanamkumbatia meya kwa maslahi yao binafsi.
 
Bila kutaka majina yao yatajwe walisema Meya ni mmoja wa viongozi ambao wanataka kuifilisi halmashauri ya manispaa ya Bukoba, walisema wanachokipinga ni kwamba meya huyo ni mbinafsi sana na miradi yote inayotekelezwa katika manispaa ya Bukoba anataka kutanguliza maslahi yake mbele na ndio maana kila mradi anataka mambo yasiwe wazi kwa madiwani.
 
Walimaliza kwa kutaja miradi ambayo meya huyo ametanguliza maslahi yake mbele kuwa ni pamoja na mradi wa ujenzi kuu la Bukoba, upimaji wa viwanja 5,000 na mradi wa ujenzi wa standi kuu ya mabasi ya Kyakailabwa.
 

No comments:

Post a Comment