Monday, July 29, 2013

ZIARA YA RAIS KIKWETE MKOANI KAGERA

 Kivuko kilichozinduliwa na rais Kikwete, ni cha Rusumo.
 Waziri wa maji,Jumanne Magembe akiongea na waziri wa miundo mbinu, Dkt John Magifuli.
 Magufuli na mmiliki wa mtandao huu.


SERIKALI imetoa kipindi cha wiki mbili kwa wale wanaomiliki silaha kinyume na sheria katika mikoa ya Geita, Kagera na Kigoma kuhakikisha wanazisalimisha mara moja kwa hiari ili wajiepushe na mkono wa sheria.

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokuwa akiongea na wananchi wa wilaya ya Biharamulo baada ua kuweka jiwe la msingi la uzinduzi wa ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 154 toka Kagoma hadi Rusaunga.


Kikwete amesema baada ya kipindi alichokitoa cha kumalizika serikali itaanzisha operation maalumu kusaka silaha hizo kwa kupita nyumba hadi nyumba.

Amesema operation hiyo maalumu itaendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na jeshi la polisi, jeshi la ulinzi na usalama na idara ya usalama wa taifa.
 Vikundi vya burudani.

 Mpiga picha maarufu, Issa Michuzi na mmiliki wa mtandao huu, Audax Mutiganzi.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera, kanali mstaafu Fabian Massawe,akicheza ngoma.
Jumanne Magembe akiwatunza wasanii.

No comments:

Post a Comment