Friday, July 26, 2013

RAIS KIKWETE WILAYANI BIHARAMULO

VIONGOZI wa vyama vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini wametakiwa kuja mkoani Kagera kujifunza namma chama cha ushirika cha Kagera (KCU)kinavyoendesha  shughuli zake ili waweze kupata elimu ya itakayowasaidi kuimarisha vyama vyao vya ushirika.
 
Kauli hiyo imetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Jakaya Kikwete mara kuzindua jesho la kitega uchumi lililojengwa na chama cha ushirika cha Kagera (KCU) liliko mtaa wa one way jana.
 
Rais Kikwete alisema chama cha ushirika Kagera ni moja ya vyama vya ushirika nchini ambavyo vimeimarika zaidi na vyenye uwezo mkubwa ukilinanisha na vyama vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini.

Alisema kuimarisha kwa chama hicho kunatokana na mikakati mizuri inayopangwa na viongozi wa chama hicho yenye lengo la kuiimarisha hasa kwa kikijengea uwezo zaidi.

"KCU ni chama cha ushirika ambacho ni imara kisichoteteleka na chenye mafanikio mazuri viongozi wa vyama vya ushirika ni lazima waje kupata elimu ya namna ya kuendesha vyama vyao" alisema Rais huyo.
 
Alisema vyama vya ushirika vinapoimarika vinawanufaisha zaidi wakulima kwa kuwa vinakuwa na uwezo mkuba wa kukusanya mazao toka kwa wakulima na kuwalipa kwa wakati, aliendelea kusema kwa vyama vya ushirika kamwe haviwezi kuimarika bila kuwa na nguzo.
 
Rais huyo alisema nguzo kuu ya inayiviimarisha vyama vya ushirika ni vitega uchumi, alisema vitega uchumi vinaviwezesha vyama vya ushirika kupata mikopo toka kwenye taasisi za kifedha.
 
"Nimefurahia taarifa niliyopokea toka KCU inapendeza,nimefurahishwa na idadi ya vitega uchumi vikubwa inavyovimiliki  ambavyo vinaweza kuipa dhamana popote duniani, naomba uongozi wa KCU uendelee kubuni mambo makuba zaidi" alisema.
 
Alisema serikali kila mara imekuwa ikipata mzigo mkubwa wa kuvinasua vyama vya ushirika kwa kuvilipa madeni, amesema hali hiyo ni mbaya sana kwa kuwa inaitia serikali hasara kubwa.
 
Rais Kikwete alisema sasa ni wakati wa vyama vya ushirika kijiendesha bila kutegemea ruzuku toka serikalini, utegemezi huo unawadidimiza wakulima kwa kuwa vinakuwa havina uhakika wa kukusanya mazao toka kwao na kuwalipa kwa wakati.
 
 
 





No comments:

Post a Comment