Wednesday, July 17, 2013

MSAJILI AIAGIZA MITANDAO KAGERA KUFANYA UCHAGUZI


Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini MICHAEL  KATEMBA ameiagiza mitandao yote ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA kuhakikisha inafanya uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi MITATU kuanzia sasa ili iweze kupata wawakilishi watakaoshiriki katika zoezi la kuwachagua viongozi wapya wataoongoza mtandao unaoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo (KANGONET).

Ametoa agizo hilo leo wakati wa kikao kilichowashirikisha wawakilishi wa mitandao inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kisekari toka katika wilaya zote zilizoko mkoani KAGERA kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya BUKOBA kilichokuwa na lengo la kumaliza mgogoro uliopo kati ya mitandao ya wilaya mkoani humo na uongozi wa sasa wa KANGONET.

Agizo alilolitoa KATEMBA limekuja baada ya kuelezwa na washiriki wa kikao hicho chanzo cha mgogoro ilioko kati ya uongozi wa sasa wa KANGONET na mitandao ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali  mkoani KAGERA.

Katika kikao hicho wawakilishi wa mitandao ya wilaya kwa nyakati tofauti walimweleza , KATEMBA kuwa  mgogoro ulipo kati ya mitandao wilaya na  KANGONET  kwamba  unachangiwa na tabia  ya baadhi ya viongozi wa sasa ya  kutaka kujinufaisha kupitia katika mtandao huo na  kutokataka kuitisha mikutano na uchaguzi kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa KANGONET na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (KADETFU) linalotuhumiwa kupora majukumu ya KAGONET, YUSTO MCHURUZA, katika kikao hicho amesema shirika lake la KADETFU kuwa  halina mahusiano na mtandao wa KANGONET katika utendaji wake wa kazi, amesema mambo yanayoifanya KANGONET ishindwe kuitisha mkutano wa uchaguzi kuwa ni pamoja na ukata unaokabili mtandao huo.

No comments:

Post a Comment