Tuesday, June 11, 2013

WADAU WA SEKTA YA UVUVI WAWEKA MIKAKATI YA KUIMARISHA UVUVI BORA NA ENDELEVU MKOANI KAGERA


Wadau wa Sekta ya Uvuvi mkoani Kagera wakutana na kuweka mikakati mbalimbali ya kuendeleza uvuvi mkoani hapa kwa kuwanufaisha wanakagera na kuzingatia njia bora za uvuvi.
Kikao hicho kilikuwa na lengo la kujadili jinsi ya   kuuendeleza uvuvi bora katika mkoa wa Kagera aidha kubani changamoto zilizopo katika sekta hiyo na jinsi ya kuzitatua ili kuwepo na uvuvi wenye tija.
Wajumbe wa kikao hicho walijadiliana hasa jinsi ya kuendelea kutatua changamoto za bei ya samaki kati ya wavuvi na wawekezaji (wamiliki wa viwanda vya Kagera Fish na VicFish)  katika sekta hiyo ili kuinua maisha ya mvuvi wa mkoa Kagera.
Wawekezaji walishauriwa kupanga bei zao na wavuvi kwa makubaliano ambapo hawatatakiwa kuvunja makubaliano hayo  bila kuwasiliana tena na wateja wao ambao ni wavuvi ili kila mmoja ardhie bei husika.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera mabaye aliwakilishwa na Katibu Tawala Msaidi Utawala  Bw. Richard Kwitega aliwasistiza wajumbe katika hotuba yake kuendelea na mikakati ya kupambana na uvuvi haramu, utoroshaji wa mazao  ya samaki pia kupambana na wavuvi wanaovua samaki wachanga.
Pia alisistiza sana juu ya uchafuzi wa mazingira miaroni ambako samaki wanafikia baada ya kuvuliwa ziwani. Mhe. Massawe aliwaasa na kuwakumbusha viongozi wa Halmashauri husika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.
Kwa upande mwingine katika kikao hicho wajumbe waliweza kupata elimu juu ya “MAPANKI” masalia ya samaki baada ya kuondolewa minofu jinsi yanavyotengenezwa kama kitoweo na chakula cha mifugo na kutoa ajira kwa vijana  pia kusafirishwa nchi za nje na kupata fedha za kigeni.
Angalizo, wajumbe wa kikao hicho walitoa angalizo juu ya viongozi wa kisiasa kutoingilia utendaji wa watendaji wa serikali katika kufanya kazi zao pale wanaposimamia sheria mfano uvuvi haramu na uchafuzi wa mazingira miaroni.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013

No comments:

Post a Comment