Saturday, May 18, 2013

VODACOM TANZANIA KUZINDUA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA FISTULA DUNIANI MKOANI KAGERA – MANISPAA YA BUKOBA


Kampuni ya Simu ya Vodacom Tanzania yajipanga  kuzindua wiki ya Maadhimisho ya Siku ya FISTULA duniani Mkoani Kagera kesho Ijumaa tarehe 17/05/2013 katika Manispaa ya Bukoba maeneo ya Soko Kuu.

Siku ya FISTULA huadhimishwa  duniani  Mei, 23 kila mwaka na kuhamasisha wahanga wa ugonjwa huo unaotibika kujitokeza kutibiwa bure na kuutokomeza ugonjwa huo.

Uzinduzi wa wiki ya Maadhimisho ya Siku ya FISTULA duniani mkoani Kagera umeratibiwa na Vodacom Tanzania chini ya Meneja Uhusiano wa Nje Bwana Salum Mwalimu.

AKiongea na Katibu Tawala Mkoa Bw. Nassor Mnambila ofisini kwake,  Salum Mwalimu alisema, uzinduzi huo unalenga kuwahamasisha wanawake wenye tatizo la FISTULA kujitokeza ili watibiwe na matibabu ni bure.

Ugonjwa wa FISTULA unatibiwa katika Haspitali ya CCBRT iliyopo Jijini Dar es Salaam na matibabu hayo hutolewa bure. 

Aidha kwa wanawake wenye matatizo hayo walioko mikoani wanatakiwa kujitokeza na kuijiandikisha ambapo watasafirishwa bure na kutibiwa bure katika hospitali hiyo.

Katika uzinduzi huo watakuwepo wasanii mbalimbali, Mabalozi wa FISTULA (waliotibiwa tatizo hilo na kupona) Madaktari mbalimbali na wawakilishi wa Vodacom Tanzania pamoja na wananchi wanakaribishwa.

Vodacom Tanzania wanasaidia na kuchangia katika matibabu ya FISTULA yanayotolewa bure katika Hospitali ya CCBRT Dar es Salaam. Aidha, wachangia gharama za matibabu ili kumaliza tatizo la FISTULA katika jamii kama mojawapo ya huduma zao kwa jamii ya Watanzania.

Uzinduzi huo baada ya kufanyika rasmi mkoani Kagera kesho tarehe 17/05/2013 pia utapitia mikoa ya Geita, Mwanza, Singida, Dodoma, Pwani na Dar es Salaam.
Imeandaliwa na:
Sylvester Raphael
AFISA HABARI
RS-KAGERA@2013



No comments:

Post a Comment