Thursday, May 23, 2013

BALOZI DR. KAMALA AENDELEA KUINADI TANZANIA

 Balozi wa Tanzania BANELUX na Jumuiya ya Ulaya Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiweka sahihi Hati ya Makubaliano na taasisi ya Uholanzi ya SANEC kwa ajili ya SANEC kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania BENELUX kutekeleza Sera ya Tanzania ya Diplomasia ya Uchumi. Kushoto ni Bwana Mark Agterdenbosch Meneja Mkuu wa SANEC. Uwekaji sahihi umefanyika leo The Hague Uholanzi.
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (mwenye tai yenye rangi ya taifa) akipeana mkono na Bwana Mark Agterdenborsh Meneje Mkuu wa SANEC baada ya uwekaji sahihi Hati ya Makubaliano ya kushirikiana kutekeleza sera ya Tanzania ya Diplomasia ya Uchumi. Shughuli ya uwekaji sahihi imefanyika leo, The Hague, Uholanzi.

No comments:

Post a Comment