Wednesday, May 08, 2013

AFIKISHWA MAHAKANI KWA KUIBA MAMILIONI

 
Mfanyakazi mwenye asilia ya kiasia wa kampuni inayojihusisha na uuzaji wa mafuta ya ABOOS iliyoko mjini BUKOBA, HAMADI ALI MOHAMED amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili za kumuibia mwajili wake RAZA FAZAL zaidi ya shilingi milioni 526.9.
 
Mtuhumiwa huyo alifikishwa leo mahakamini  kusomewa tuhuma zinazomkabili mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya BUKOBA , Mheshimiwa CHARLES  UISO.
 
Mwendesha mashitaka ambaye pia ni wakili wa serikali PAUL KADUSHI akisoma mashitaka yanayomkabili mbele ya hakimu huyo amesema mtuhumiwa anadaiwa kumuibia kiasi hicho cha fedha mwajili wake kwa nyakati tofauti kati ya mwezi  JANUARI hadi DESEMBA mwaka 2010.
 
Mtuhumiwa huyo alikana mashataka yote aliyosomewa, pamoja na dhamana  kuwa wazi mtuhumiwa huyo alikosa watu wa kumdhamini  hivyo alipelekwa gerezani, kesi ya mtuhumiwa huyo itatajwa tena   juni  23, mwaka huu.
 
Mtuhumiwa huyo alikamatwa jana na jeshi la polisi mkoani KAGERA lililokuwa likimsaka wakati akiwa  kwenye harakati za kutoroka kuelekea  nchi jirani ambayo haikubainishwa.
 

No comments:

Post a Comment