Wednesday, April 24, 2013

SERIKALI YASHAURIWA SHULE ZINAZOIBA MITIHANI

BAADHI ya wadau wa sekta ya elimu katika mkoa wa Kagera wameishauri serikali kuzifungia kabisa shule zinazobainika kujihusisha na  wizi wa mitihani pamoja na kuwachukulia hatua za kali  baadhi wamiliki wa shule  hizo na maofisa wa serikali wanaoshirikiana nao ili iweze kukuza na kuimarisha sekta hiyo nchini.
 
Wadau sekta hiyo wametoa ushauri huo leo kwa nyakati tofauti wakati wakieleza sababu mbalimbali zinazochangia kudumaza ukuaji wa kiwango cha elimu hapa nchini.
 
 
 Walisema   kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini kunachangiwa na tabia ya kuvuja kwa mitihani, walisema  kuvuja kwa mitihani kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya  wamiliki wa shule binafsi ambao hupenda shule zao zionekane maarufu  zaidi ya shule nyingine.
 
 
Mwandishi maarufu wa vitabu hapa nchini vinavyohusiana na masuala ya kilimo Pius Ngeze ambaye pia ni  mwenyekiti wa zamani wa Chama Cha mapinduzi (CCM) wa mkoa wa Kagera alisema wamiliki wa shule wanaoshirikiana na baadhi ya maofisa wa baraza la mitihani kuiba mitihani kwamba wanaua nchi.
 
 
 Ngeze aliwafananisha  ya wamiliki wa shule wanaowapa majibu wanafunzi ili shule zao zionekane zinafanya vizuri sawa na wauwaji, alisema mmiliki wa shule anayewampa wanafunzi majibu ya mtihani ili shule yake ionekana inafanya vizuri  kuwa anakuwa anawamchimbia kaburi.
 
 
Leonidas Mgashe,  ambaye ni afisa utalii wa kampuni ya utalii ya walkgard  iliyoko mkoani  Kagera anasema kuna  baadhi ya wamiliki wa shule binafsi wanaotaka shule zao zionekane maarufu zaidi ya shule nyingine, aliwatuhumu kuwa wamiliki hao ndio wanajihusisha na vitendo vya wizi wa mitihani ili shule zao zifanye vizuri waweze kupata wateja wengi zaidi.
 
 
 
Naye, mwenyekiti wa baraza la usafiri wa majini na nchi kavu mkoani Kagera, Michael Cleophace alitoa ushauri kwa  watendaji wa baraza la mitihani kuzingatia  maadili ya kazi yao ili wajiepushe na vishawishi waweze kuinua na kuimarisha kiwango cha elimu hapa nchini.
 
 
Alimaliza kwa kuiomba serikali kubuni mikakati itakayosaidia kuthibiti mianya yote inayochangia kuvuja kwa mitihani inayotungwa na baraza la mitihani.
 
 

No comments:

Post a Comment