Monday, April 01, 2013

KAMANDA KALANGI AKIELEZEA MATUKIO YA UHARIFU

 
MTU mmoja anayetuhumiwa kwa  ujangili ameuwawa baada mapambano makali ya kurushiana risasi kati ya askari jeshi  la polisi mkoani Kagera lililoshirikiana na askari wa idara ya wanyama pori na kundi la watuhumiwa wa ujangili ndani ya pori la hifadhi ya taifa la Burigi lililoko wilayani Ngara.

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi amesema mapambano hayo yalianza pale majangili hayo yaliyokuwa na silaha mbalimbali za kivita yalipoanza kujiami kwa kwa kuwarushia askari risasi ambao walikuwa wakiyaamulu majangili hayo yajisalimishe.


Katika tukio jingine kamanda Kalangi amewaambia waandishi wa habari kuwa jeshi la polisi linamshikilia Joshua Mlindwa (25) mhaya mkazi wa kata kashai mhutumiwa wa kuvunja ofisi ya shule ya sekondari  ya Bukoba kwa kutumia funguo bandia  kuiba yeti vya taaluma 131.

Akisimulia tukio hilo amesema mtuhumiwa amekamatwa baada ya kuwekewa mtego,  Kalangi amesema kuwa mtuhumiwa alikuwa akidai uongozi wa shule ya sekondari ya Bukoba impatie shilingi milioni 6 ambayo alitaka ilipwe kwa njia ya M pesa ili aweze kurejesha vyeti hivyo la sivyo angeviaribu kwa kuvichoma moto.
 Kamanda Kalangi akionyesha vyeti ambavyo vilikuwa vimeibiwa na mtuhumiwa anayeshikiliwa na jeshi la polisi n i vyeti vya taaluma vya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya Bukoba iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
Kamanda akionyesha funguo bandia.

No comments:

Post a Comment