Monday, March 04, 2013

CCM YAMUWEKA NJIA PANDA MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA ANATORY AMANI

MEYA wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba Anatory Amani  ameendelea kukumbana na wakati mgumu, hii inafuatia hatua ya Chama Cha mapinduzi kuunga mkono juhudi  zinachukuliwa na kundi la baadhi ya madiwani wa manispaa hiyo za kutaka kumg'oa Meya huyo.

Katika hali isiyo ya kawaida Katibu wa itikadi, siasa na uenezi ya CCM, Nape Mnauye  ameiagiza wizara ya TAMISEMI kuunda tume maalumu itakayochunguza tuhuma zinazomkabili meya huyo zinazohusiana na masuala ya ubadhilifu.

Kwa kauli yake Mnauye alisema CCM imefikia hatua ya kuagiza kuundwa kwa tume hiyo baada ya kupata maelezo mbalimbali yanayohusu tuhuma zinazomhusu Meya huyo.

Alisema tume hiyo itakuwa huru na itatoa taarifa hadharani baada ya kumaliza kazi yake, aliendelea kusema yoyote atakayebainika na kosa lolote kufuatia uchunguzi wa tume hatua dhidi yake zitachukuliwa.

Nape alizitaja tuhuma mbalimbali zinazomkabili Meya huyo kuwa ni pamoja na mikataba ya ujenzi wa soko kuu la Bukoba, standi kuu ya mabasi, upimaji wa viwanja 5,000 na miradi mingine ambayo ni pamoja na ujenzi wa jengo la kitega uchumi.

No comments:

Post a Comment