Thursday, March 21, 2013

BALOZI WA TANZANIA NCHINI UBELGIJI ATOA MWALIKO



Mhe. Dkt. Diodorus Buberwa Kamala, Balozi wa Tanzania Ubelgiji, Uholanzi, Luxembourg na Jumuiya ya Ulaya anayo furaha kuwaalika Watanzania wote wanaoishi katika nchi za Ubelgiji, Uholanzi na Luxembourg kushiriki Tamasha la Filamu za Afrika ambalo litakuwa na siku mbili maalum za kuonyesha Filamu za Kitanzania. Filamu ya Kitanzania inayojulikana kwa jina la “A Teachers Country” itaonyeshwa  tarehe 29/03/2013 katika ukumbi wa sinema wa KINEPOLIS, Bondgenotenlaan 145, Leuven kuanzia saa mbili usiku. Aidha, tarehe 30/03/2013 Filamu za Kitanzania zinazojulikana kwa majina ya  “ The Road to Sainthood na Mwalimu: The Legacy of Julius Kambarage Nyerere”  zitaonyeshwa katika ukumbi wa Museum M, Leuven, Ubelgiji kuanzia saa 5.30 Asubuhi. Mhe. Madaraka Nyerere atakuwa mgeni rasmi.
Wote mnakaribishwa kuja kushiriki katika Tamasha la Filamu za Kitanzania.

Imetolewa na Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Balozi wa Tanzania – BENELUX
21/03/2013

No comments:

Post a Comment