Sunday, February 03, 2013

RAIS KIKWETE ABARIKI UTARATIBU WA VITAMBULISHO VYA TAIFA

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akitia saini baada ya  kuthibitisha maelezo yake binafsi kwenye Fomu ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho hicho  nyumbani kwake jijini Dar es salaam  leo, Ijumaa, Februari Mosi, 2013. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Bwana Dickson E Maimu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akipiga picha kwa ajili ya Kitambulisho cha Taifa wakati alipokamilisha taratibu za kupatiwa Kitambulisho cha Taifa nyumbani kwake.

No comments:

Post a Comment