Sunday, February 03, 2013

Na Anderson Mujwahuzi.

PEPO mbaya ameendelea kuvuma ndani ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba iliyoko mkoani Kagera, hii inafuatia hatua ya mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Anatory Amani ya kupeleka mjini Dodoma mapendekezo ya awali ya bajeti ya mwaka 2013/14 bila kujadiliwa na madiwani wa manispaa hiyo.

Madiwani walioongea na mtandao huu kwa nyakati yofauti wamesema kuwa uamzi wa meya wa kupeleka mijini Dodoma bajeti ambayo haijajadiliwa na madiwani kuwa inaonyesha jinsi gani anavyotaka kuifilisi manispaa hiyo.

"Huyu bwana ni fisadi mkubwa sana na ndio maana tunampinga, amekataa kuitisha kikao cha baraza la madiwani cha kujadili bajeti kwa hofu ya kuhofia kuibuka kwa mjadala wa tuhuma zinazomkabili za ubadhilifu" alisema mmoja wa madiwani.

Baadhi ya madiwani wamesema bajeti ambayo Mstahiki Meya ameipeleka Dodoma kuwa hawatakubakiana nayo, wamesema bajeti hiyo ni yake binafsi, "haiwezekani mtu ukakataa kuitisha vikao muhimu  kwa hofu ya kung'olewa, kinachotia aibu ni hatua yake ya kuweka pingamizi mahakamani ili vikao visifanyike.

No comments:

Post a Comment