Wednesday, January 23, 2013

MBIVU AU MBICHI KATI YA BALOZI KHAMIS KAGASHEKI NA MEYA WA MANISPAA ANATORY AMANI

 Na Mwandishi wetu

LEO ndio siku itakayotoa hatima ya mgogoro ulipo kati ya Balozi Kagasheki ambaye ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini na Anatory Amani ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba.

Halmashauri kuu ya wilaya aya Bukoba mjini (CCM) itakaa kikao cha dharura kitakachofanyika kwenye ukumbi wa mtakatifu Francis chenye lengo la kujadili hatima ya Meya Amani, katika kikao wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Bukoba watapiga kura za kumkubali au kumkataa Meya Anatory Amani.

Umazi wa kutaka kumg'oa Meya madaraka unadaiwa kufuatia hatua yake ya kutaka kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo kwa maslahi yake binafsi.

Kikao hicho kitahudhuliwa na makamu mwenyekiti wa Chama  Cha Mapinbduzi taifa, Philip Magula ambaye ameishawasili mkoani Kagera tangu jana, katika hali ambayo sio ya kawaida pande zote zinazopingana kila moja ilikuwa ikitamba kuibuka mshindi katika sakata hilo.


No comments:

Post a Comment