Friday, January 18, 2013

HITIMISHO LA MAFUNZO KWA WAKINA MAMA WAJANE NA WALEZI WA WATOTO YATIMA

 Askofu msaidizi wa jimbo la Bukoba, Methodius Kilaini akifungua cheti maalumu kilichotolewa kwa wakina mama walioshiriki kwenye maonyesho ya wajasiliamali yaliyofanyika mkoani Shinyannga, kulia kwake ni Gozibert Kaserwa mratibu wa shirika la uwezeshaji kwa wanawake na watoto la matumaini mapya.
Shamra shamra za  hitimisho la mafunzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Bukoba iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
 Baadhi ya wahitimu wa mafunzo.
 Askofu Kilaini akitoa ruzuku kwa wahitimu wa mafunzo ya ujasiliamali yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la matumaini mapya, zaidi ya wakina mama wajane, watoto , na wanaolea watoto yatima 80 wamenufaika na rizuku hiyo, ambapo kila aliyenufaika atapata shilingi 240,000 za kuanzisha shughuli mbalimbali za kuwapatia kipato.
 Wahitimu wa mafunzo yaliyotolewa na shirika lisilo la Kiserikali la matumaini mapya wakiwa katika picha ya pamoja na askofu Methodius Kilaini.


No comments:

Post a Comment