Thursday, January 03, 2013

CHANJO ZA NIMONIA NA KUHARISHA ZAZINDULIWA RASMI MKOANI KAGERA.

 Baadhi ya wazazi waliowaleta watoto kwa ajili ya chanjo.

Na Syliverster Raphael- afisa habari wa mkoa wa Kagera

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe.Kanali Mstaafu Fabian I.  Massawe azindua rasmi chanjo ya Nimonia na Kuharisha kwa watoto chini ya miaka mitano (U 5) mkoani Kagera. Uzinduzi huo umefanyika januari 3,2013 katika Kituo cha Afya cha Rwamishenye Manispaa ya Bukoba.

Katika uzinduzi huo wa chanjo mpya  za Nimonia na Kuharisha  ambazo zinatolewa kwa mara ya kwanza nchini ukiwemo mkoa wa Kagera unaotegemea kuchanja jumla ya  watoto wapatao 109,407 kwa wilaya zote saba,  takwimu hizo zilitolewa na Dk. Salum I.Sufiani Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa katika uzinduzi hizo mpya.

Aidha Mhe. Massawe kabla ya kuzindua chanjo hizo aliwaasa wazazi (akina mama) walioleta watoto wao kwa ajili ya kuchanjwa kuzingatia uzazi wa mpango na kuachana na  tamaduni za zamani,  “Kwa sababu zamani hakukuwapo na chanjo za aina mbalimbali, wazazi walizaa watoto wengi ili wakifa, watoto wengine wabaki lakini sasa chanjo za kuzuia vifo vya watoto zipo” Alisistiza Mkuu wa Mkoa.

Pia Mkuu wa Mkoa alisistiza ubora wa chanjo hizo za Nimonia (Uti wa Mgongo) na kuharisha kuwa zina viwango vinavyotakiwa na hazina madhara, zimethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Wananchi walisistizwa kuhakikisha watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wanachanjwa bila kuhofia chanjo hizo.

Vilevile Mhe. Massawe aliwaomba wazazi kuzingatia ratiba ya chanjo hizo ambapo chanjo ya kuharisha inatakiwa mtoto apewe dozi ya kwanza ndani ya wiki 15 tu na dozi ya pili apewe mtoto ndani ya wiki 32 tu. Aidha chanjoa ya Nimonia mtoto anatakiwa kupewa katika wiki ya 6, wiki 10 na wiki ya 14 tu.

Kutokana na magojwa ya kuharisha kusabibishwa na uchafu, Mkuu wa Mkoa hakusita kuwasistiza wananchi wa Kagera kudumisha usafi katika maeneo yao hasa hasa wakina mama wenye watoto wachanga. Pia aliwashukuru wakazi wa Manispaa ya Bukoba kwa kuuweka mji wao katika hali ya usafi unayoridhisha.

No comments:

Post a Comment