Monday, December 10, 2012

TAKUKURU KAGERA YAADHIMISHA SIKU YA MAADILI KWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA

 Kamanda wa TAKUKURU mkoani Kagera, Bi. Domina Mukama (kulia) mara baada ya kuwasili kwenye eneo la kituo cha kulelea watoto yatima cha Nusuru Yatima kilichoko katika manispaa ya Bukoba.
 Bi. Mukama akikabidhi sehemu ya msaada uliotolewa na TAKUKURU Kagera kwa mlezi wa kituo hicho Bi. Saada Khamis, Taasisi hiyo ilitoa misaada ambayo ni pamoja na vyakula na sabuni za kuoga, Bi. Mukama alionyesha kusikitishwa na mazingira ya wanapolelewa watoto hao yatima hivyo akaiomba jamii ijenge utamaduni wa kuyasaidia makundi yasiyojiweza hasa yenye uhitaji zaidi.
 Baadhi ya watoto yatima walionufaika na msaada uliotolewa na TAKUKURU Kagera wakishangilia, kituo hicho kinatunza watoto yatima zaidi ya 30.

No comments:

Post a Comment