Tuesday, November 06, 2012

VIONGOZI WA MADHEHEBU YA DINI WAKUTANA NA MKUU WA MKOA WA KAGERA MASSAWE NA KUWEKA MIKAKATI YA KUDUMISHA AMANI

  Mkuu wa Mkoa Akiongea na Viongozi wa Dini Kwa Kutoa Mifano  Mbalimbali Ubaoni Jinsi Ambavyo Serikali Inashirikiana na Dini Kulinda Amani.
 
 Mmoja wa kiongozi wa madhehebu ya dini ya kiislamu.
 Askofu wa kanisa la kiinjili la Kirutheri diosisi ya kaskazini magharibi Elisa Buberwa.

Viongozi wa dini Mkoani Kagera waweka mikakati ya pamoja ya  kudumisha amani upendo na ushirikiano pia kuhakikisha wanawahubiria waamini wa dini zao kujiepusha na vitendo vinavyoweza kuvuruga na kuhatarisha  amani ya Mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla.
Mikakati hiyo iafikiwa katika kikao cha pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Kagera aliyeitisha kikao hicho leo tarehe 5/11/20212  ili kujadili na kuweka  mikakat i ya  kuendeleza amani katika mkoa wa Kagera kutokana na viashiria vya uvunjifu wa amani vilivyoanza kuonekana katika baadhi ya maeneo mbalimbali Tanzania.
Mkuu wa Mkoa akiongea na viongozi hao aliwasistiza kuwa serikali na dini ni vyombo ambavyo vinategemeana katika kudumisha amani ya nchi. Viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kuhakikisha inchi inakuwa na amani.
Mhe. Massawe alisistiza juu ya baadhi ya viongozi wa madhehebu ya dini kuacha kufanya miadhara ya kukashifu madhehebu na dini za wenzao ambapo kila dhehebu au dini imetakiwa kuhubiri na kutoa mafundisho yanayoihusu dini hiyo yenyewe.
Wakitoa maoni yao juu ya kudumisha amani na upendo katika mkoa wa Kagera na Tanzania kwa ujumla viongozi hao walipendekeza serikali kutafuta vyanzo vya machafuko ya dini kuliko kushughulika na matokeo, pia serikali kuhakikisha inavisajili vikundi vyote ambavyo vipo chini ya dini husika.
Aidha  viongozi hao  wametoa wito kwa serikali kuwa wananchi wanaofanya vitendo vya kukashifu vitabu vitakatifu wachukuliwe hatua za kisheria kama wao wenyewe na siyo kuwa dini zao zinawatuma kutekeleza uhalifu huo kwa baadhi ya dini za wenzao.
Pia viongozi wa dini mkoa wa Kagera wamesistiza kuwa dini isiwe kichaka cha kuficha maovu ya watu wanaopenda kuficha uovu wao kwa mgongo wa dini. “Baadhi ya watu wanaofanya maovu ya kuchoma nyumba za  ibada wachuliwe hatua na serikali mara moja na wasizifanye dini kuwa vichaka vya kuficha uovu wao.” Alisistiza Askofu Method Kilaini Jimbo Katoliki la Bukoba.
Katika Kufunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa amewaomba viongozi hao wa dini kushirikiana na serikali kulitafutia ufumbuzi suala la ajira za vijana ambapo amewahimiza viongozi hao kuanzisha vyuo mbalimbali vya ufundi vya kuwafunza vijana kujitegemea  na siyo kuisubiri serikali kuwaajili. Aidha amewahimiza viongozi hao kuwahubiri wananchi wa Kagera kufanya kazi na kuacha uvivu ili kujipatia kipato.

No comments:

Post a Comment