Saturday, November 24, 2012

MKUTANO WA HADHARA ULIOANDALIWA NA WAZIRI KAGASHEKI

 Balozi Khamis Kagasheki akipongezwa na wananchi baada ya kumaliza hotuba yake ya mkutano wa hadhara aliouandaa uliofanyika kwenye viwanja vya uwanja wa uhuru.




 


WAZIRI wa maliasili na utalii Balozi Khamis Kagasheki ameutaka uongozi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuweka wazi mikataba inayoiingia inayohusu miradi ya maendeleo inayobuniwa na manispaa hiyo  kabla ya kuanza kuteikeleza.



Alisema wakiweka wazi mikataba ya miradi ya maendeleo inayobuniwa na uongozi wa manispaa hiyo kabla ya kuitekeleza watakuwa wanajenga imani kuwa ya wananchi ambao ni sehemu ya miradi inayobuniwa.



Balozi Kagasheki alitoa kauli hiyo alipokuwa akiwahutubia wananchi wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye maeneo ya viwanja vya uhuru vilivyoko katika manispaa hiyo.



Alisema baadhi ya miradi ambayo manispaa inataka kuitekeleza ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu jipya la Bukoba na upimaji wa viwanja 5,000 kuwa mikataba yake haileweki na haiku wazi, “mimi kama mbunge na diwani wa manispaa ya Bukoba sijawahi kuonyeshwa mkataba aina yoyote naisikia kama watu wengine” alisema waziri.



“Sioni haja ya uongozi wa manispaa ya kuficha mikataba ya mradi unaotaka kuitekeleza, hali hii inaonyesha ndani ya mikataba hiyo palivyo na ajenda ya siri, haiwezekani mambo ya wananchi yafanyike kwa uficho mkubwa, na mimi sitakubali mambo yafanyike kwa uficho mkubwa nitahakikisha kila kitu kinakuwa wazi” alisema huku wananchi wakimshangilia kwa nguvu.



Waziri huyo alisema tunaposhindwa kuweka mambo wazi tunakuwa tunawapa wapinzani nafasi ya kutujadili, “sasa natamka kuwa soko halitavinjwa januari 15, mwaka kesho kama uongozi wa manispaa unavyotaka kufanya kupisha ujenzi wa soko kuu jipya la kisasa hadi  tuhakiki mikataba ambayo imefichwa, hapa ,kina kitu”  alisema kwa msisitizo.



Aliuagiza uongozi wa manispaa kabla ya kuwaondoa wafanyabiashara walioko ndani ya soko kuwatafutia sehemu mbadala ambayo wataitumia kufanya biashara wakati ujenzi wa soko ukiendelea.



“Nashangaa kuna baadhi ya viongozi walioko ndani ya manispaa wanaosambaza habari kuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa ya Bukoba, Naapa sipingi maendeleo ila ninachotaka ni kila  kifanyike kwa kufuata taratibu zilizowekwa za utekelezwaji wa miradi ya maendeleo inayobuniwa, hatutaki watu wabuni miradi na waitekeleze kulingana na matakwa yao” alisema Balozi Kagasheki.



“Ningekuwa napinga mambo ya maendeleo ndani ya manispaa nisingerekebisha soko sehemu wanapouzia ndizi, nisinge jenga vyumba vya madarasa karibu kila kata, nisingeweka taa za barabarani na mambo mengine makubwa, wanaosema ninapinga maendeleo inaonekana wana mazazo mgando” alisema.



Alimaliza kwa kuwaomba wananchi wa manipaa ya Bukoba waimarishe mshikamano ili waweze kupambana na vitendo vya kidharimu vinavyochangia kuvuruga amani ndani ya manispaa hiyo.





 Mstahiki meya wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba akiondoka kwenye jukwaa baada ya mkutano.
 Viongozi wa dini walikuwa miongoni mwa walioudhuria mkutano huo, anayempongeza balozi Kagasheki ni Padre Projestus Mutungi wa kanisa Katoriki.


 Baadhi ya vijana wakisukuma gari alilokuwemo Balozi Kagasheki, wa.lifanya hivyo baada ya kukunwa na hotuba yake aliyoitoa.
Wasanii wa kikundi cha sanaa cha KAKAU wakifanya vitu vyao.

No comments:

Post a Comment