Tuesday, November 20, 2012

JESHI LA POLISI MKOANI KAGERA LILIVYOFANIKIWA KUNASA SILAHA ZA KIVITA ZILIZOKUWA ZKITUMIKA KUTEKELEZA UJAMBAZI

 Silaha zilizokamatwa na jeshi la polisi mkoani Kagera.

 Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari wakisikiliza kwa makini taarifa ya jeshi la polisi mkoani kage ya kukamata silaha aina ya SMG iliyokuwa inatumika kutekeleza matukio ya uharifu mkoani Kagera.
 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi akitoa taarifa juu ya operation ya jeshi la polisi iliyozaa matunda ambayo ni kukamata silaha ya kivita aina ya SMG iliyokuwa inamilikiwa na Hassan Majura na Godlove Benezeth wote wakazi wa kata ya kashai iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
JESHI la polisi limefanikiwa kukamata silaha ya kivita aina ya SMG iliyokuwa inatumiwa na majambazi kutekeleza matukio makubwa ya  uharifu kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.
Kukamatwa kwa silaha hiyo aina ya SMG kulidhihirishwa na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Philip Kalangi alikutana na waandishi wa habari ofisini kwake jana.

Akisimulia tukio la kukamatwa kwa silaha hiyo Kalangi alisema kuwa jeshi hilo lilikamata silaha hiyo Novemba 17, mwaka huu, alisema silaha hiyo ilikuwa imefichwa kwenye eneo la kijiji cha Bwagale kilichopo wilaya ya Bukoba vijijini ikiwa na magazini mbili na risasi zaidi ya 20.

Alisema silaha hiyo ilikuwa inamilikiwa na watuhumiwa wa  ujambazi aliowataja kwa majina kuwa ni pamoja na Hassan Majura (35) na Godlove Benezeth (34) wakazi wa kata Kashai ambao kwa pamoja hadi sasa wanashikiliwa na jeshi hilo kwa ajili ya mahojiano.

Kalangi alisema mahojiano ya awali kati ya jeshi la polisi na watuhumiwa hao yanaonyesha kuwa walikuwa wanaitumia silaha hiyo kutekeleza uharifu kwa kushirikiana na raia wa nchi jirani ambayo hatuitaja, alisema inaonyesha kuwa matukio mengi yaliyokuwa yanatokea wilayani Missenyi yalikuwa yanaratibiwa na watuhumiwa hao.

Aliendelea kusema kuwa watuhumiwa wote walikuwa na mtandao mkubwa wa ujambazi kwa kuwa walipopekuwa kwenye makazi yao walikutwa na sare za kijeshi ambazo hadi sasa hazijatambuliwa zilitokea nchi ipi.

Aliwaambia kuwa jeshi la polisi lilifanikiwa kuwanasa watuhumiwa na silaha waliyokuwa wakihimiliki baada ya kupata taarifa za siri toka kwa wananchi walioshindwa kuelewa nyendo zao.

Aliwashukuru wananchi waliotoa taarifa kwa jeshi hilo ambazo zmelisaidia kunasa silaha iliyokuwa inatumika kutekeleza matukio mengi ya uharifu mkoani Kagera, aliwaomba wananchi waendelee kutekeleza dhana ya polisi jamii.

 Kalangi akionyesha sare za jeshi ambazo hazijulikani za nchi gani zilizokuwa zikitumiwa na jambazi waliokamatwa.
Silaha bandia iliyotumiwa na majambazi kumtishia mfanyabiashara mwenye asili ya kihindi, ilikuwa imetengenezwa kwa miti.

No comments:

Post a Comment