Tuesday, October 09, 2012

UONGOZI WA YANGA WAKANUSHA HABARI ZA UZUSHI

 Mchezaji wa yanga Osca Joshua akiwa ndani ya chumba chake.
 Wachezaji wa timu ya YangaOmega na Frank wakiwa wamejipumzisha ndani ya vyumba vyao.
 Meneja wa hoteli ya Smart ambayo wachezaji wa timu ya yanga walikuwa wamefikia.




Na Mwandishi wetu maalumu

VIONGOZI, wachezaji wa timu ya Yanga African na uongozi wa hoteli ya Smart ambayo hiyo ilikuwa imefikia ilipokuwa mkoani Kagera kucheza ligi kuu ya vodacom na timu ya Kagera sugar wamepinga vikali  taarifa zilizochapishwa kwenye moja ya  chombo vya habari.

Kwa nyakati tofauti wakati wakiongea na vyombo mbalimbali vya habari vilivyoko mkoani Kager wamesema sio kweli kwamb wachezaji wa timu hiyo uongozi uliwalaza mzungu wa  nne yaani chumba kimoja kwa wachezaji wa nne.

Walisema taarifa hizo sio sahihi kuwa zinalenga kuugawa uongozi wa timu hiyo na washabiki wake pamoja na wanachama, kiongozi  wa msafara wa timu hiyo Tito Osollo aliwaambia waandishi wa habari kuwa chumba kimoja kilikuwa kinatumiwa na wachezaji wawili tu.

“Walioandika habari hizi wanatumiwa haiwezekani mwandishi akaandika habari kuwa sababu za timu ya Yanga kufungwa na Timu ya Kagera Sugar kwamba zimechangiwa na wachezaji wane kulala chumba kimoja” alisema.

“Mwandishi aliyeandika habari hizi hafai kabisa ni mwongo na ninawaomba wanachama na mapenzi ya timu ya Yanga kumpuuza , hayuko makini na kazi yake hivyo anafanya kazi kwa matakwa ya wanaomtumia” alisema Osollo kwa hasira.

Alisema Club ya yanga kamwe haitawavumulia waandishi wanaotaka kuchonganisha wachezaji, wapenzi, wanachama na viongozi wa timu hiyo, “ Tumefungwa, unaposhindana tegemea mambo mengi kushinda, kushindwa na kutoka sare” alimaliza.

Kutokana sakata hilo meneja  wa hoteli ya Smart ameahidi kumfikisha mwandishi wa habari aliyeandika habari za upotoshaji kuwa wachezaji wa nne wa timu ya Yanga walikuwa wanalala ndani ya chumba kimoja.

“Nimeishawasiliana na mwanasheria wetu tunaandaa hati ya madai, mwandishi huyu nitamdai fidia ya shilingi bilioni 2 , ameidhalilisha hoteli yangu, sasa namshughulikia ipasavyo, nitamshtaki kama yeye sio chombo, chomo hakikumtuma aandike habari za uongo” alisema kwa msisitizo.

Nao wachezaji wa yanga walioongea kwa nyakati tofauti walikanusha taarifa hizo kwa kusema kuwa uongozi wa klabu ya Yanga haukuwalaza wachezaji wane kwenye chumba kimoja.

No comments:

Post a Comment