Thursday, October 04, 2012

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitambulisha ujumbe wake kwa Gavana Jenerali wa Canada Mhe. David Johnson na mkewe Mama Sharon Johnson katika viwanja vya jumba la Rideau Hall  jijini Ottawa, Canada, katika hatua yake ya kwanza ya  ziara rasmi ya siku mbili jijini humo Jumatano Oktoba 4, 2012.Jumba hilo ndilo makazi  na ofisi rasmi ya Gavana Jenerali wa Canada tangia mwaka 1867 ambapo pamoja na kuishi humo pia hapo ndipo hutumika kwa kuwatunukia wananchi wa Canada waliofanya vyema, pa kupokelea wageni mashuhuri wa nchi za nje na pia ndipo anapofanyia shughuli zote za kitaifa akiwa kama mwakilishi wa Malkia wa Uingereza.

No comments:

Post a Comment