Wednesday, October 17, 2012

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MKOANI KAGERA

 Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa taarifa kwa naibu waziri wa uchukuzi Charles Tibeza aliyefanya ziara ya siku moja mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi wa serikali na mamlaka ya bandari nchini wakimsikiliza Naibu waziri Tibeza.
Naibu waziri wa uchukuzi akijibu hoja za taarifa iliyotolewa na Massawe mkuu wa mkoa wa Kagera.
 Massawe (Kulia) kimsikiliza kwa makini Naibu waziri Tibeza anayefuata ni mjumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Kagera Seif Husein na kushoto ni mjumbe mwingine Fikir Kisimba.
 Mhandisi wa kampuni ya ukandarasi ya CGG- MECCO JV inayojenga uwanja wa ndege wa Bukoba, Patric Kain akitoa sababu zinazokwamisha ujenzi wa uwanja wa Ndege, mhandisi huyo alishindwa kumpa taarifa sahihi Naibu waziri Tibeza.
 Naibu waziri Tibeza akitoa maelekezo kwa kampuni inayofanya ya ujenzi wa uwanja wa Bukoba, waziri huyo alionyeshwa kutoridhishwa na taarifa kasi ya ujenzi wa uwanja huo.
 Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Naibu waziri Tibeza alipoyembelea uwanja wa ndege wa Bukoba.
 Sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba unaofanyiwa ukarabati.
Massawe akijadiliana jambo na Naibu waziri Tibeza na watendaji wengine walienda kuona hali ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.

1 comment: