Tuesday, October 16, 2012

MKUU WA MKOA KAGERA AMUUMBUA MBUNGE WA JIMBO LA NKENGE

Huyu ndiye mbunge wa jimbo la Nkenge Asumpta Mshama.

MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amepinga vikali ushauri  uliotolewa mbunge wa jimbo la Nkenge Asumpta Mshama  wa kuiomba serikali iwaruhusu wakulima wao wenyewe wajitafitie masoko wa kahawa wanayoizalisha ndani na nje ya nchi.

Massawe amesema kamwe biashara ya kahawa haitakuwa huria hivyo wakulima wataendelea na utaratibu uliowekwa na serikali wa kuuza kahawa yao kwenye vyama vya ushirika na makampuni ya yaliyosajiliwa kisheria yanayofanya kazi ya kununua kahawa toka kwao.

Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Kagera kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa uliko kwenye manispaa ya Bukoba.

Alisema kuwa wakulima wanapouza kahawa kwa njia isiyo rasmi wanakuwa wanaikosesha serikali mapato , “halmashauri za wilaya na manispaa huwa zinanufaika na mauzo ya kahawa kwa kupata ushuru tukiruhusu biashara huria ya kahawa tutakuwa tuaziua halmashauri za wilaya na manispaa” alisema Massawe.

“Sikubaliani na kauli ya mhemimiwa mbunge biashara ya kahawa kamwe haitakuwa huria, na mimi naahidi titaendelea kuwashughulikia kikamilifu wale wote wanajihusisha biashara ya magendo ya kahawa, ni lazima tuunusuru uchumi wetu” alisema huku akishangiliwa.

Massawe alisema kamwe hatamfumbia macho mtu yoyote atakayejihusha na magendo ya kahawa’ “Nitamshughulikia mtu yoyote bila kuangalia sura yake, kabila na nafasi yake aliyonayo ndani ya jamii” alisema.

Aliwataka viongozi wote washirikiane ili wawezer kuwathibiti wale wote wanajihusisha na magendo ya kahawa, alisema magendo ya kahawa inavidhoofisha vyama vya ushirika na wakulima wanaouza kahawa yao kwa njia ya magendo, “wakulima wanaouza kahawa kwa njia ya magendo wanapunjwa sana” alimaliza kusema.


No comments:

Post a Comment