Sunday, October 21, 2012

JESHI LA POLISI KAGERA LINAVYOFANYA KAZI YA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPIMA AFYA ZAO

JESHI la polisi mkoani Kagera limeanza kutekeleza mkakati wake  mpya ambao limeubuni  wa kuwahamasisha wananchi  mkoani humo kupima afya zao.

Mkakati  huo  ulidhihirika mwishoni mwa wiki baada jeshi hilo kuendesha zoezi la kuwapima wananchi wa manispaa ya Bukoba na maeneo mengine virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa UKIMWI.

Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye maeneo ya standi kuu ya mabasi zaidi ya wananchi zaidi 1,500 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI kwa hiari.

Akiongea wakati wa zoezi hilo la upimaji mrakibu msaidizi wa jeshi la polisi Dr Hussein Gamu ambayo aliendesha zoezi hilo kwa kushirikiana na maofisa wengine wa jeshi hilo alisema mkakati wa jeshi hilo wa kuanzisha utaratibu wa kupima wananchi afya zao unalinga kuimarisha mahusiano kati ya jeshi hilo na wananchi.

Gamu alisema jeshi la polisi lina mkakati mkikati  ya kuimarisha ustawi wa wananchi, alisema wananchi wanapokuwa na ustawi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu yao vizuri.

Afisa huyo alisema kuwa wananchi ndio nguzo kubwa ya  jeshi la polisi, aliendelea kusema wananchi ndio wanalipa nguvu jeshi hilo liweze kutekeleza majukumu yake vizuri.

Alisema taarifa zinazotolewa na wananchi zinazohusiana na masuala ya uharifu kuwa  ndizo zinazolisaidia jeshi la polisi kukabiliana na matukio ya uharifu kwa kiasi kikubwa.

Gamu alisema jeshi hilo litaendelea kuwa karibu na wananchi hasa kupitia kwenye dhana yake maalumu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi, alimaliza kwa kuwaomba wananchi waendelee kulipa ushirikiano jeshi hilo ili waweze kunufaika nalo zaidi.

No comments:

Post a Comment