Tuesday, December 12, 2017
Tuesday, July 19, 2016
MAJALIWA: MALIASILI NA UTALII JIPANGENI VIZURI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii
kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa.
kujipanga vizuri na kufanya mapitio ya idara zake hususan ya misitu baada ya kubainika kuwepo kwa matatizo makubwa.
“Eneo la misitu limekuwa na
matatizo makubwa, watendaji wengi si waaminifu na sura ya wizara si nzuri miti
mingi inakatwa na fedha haiingii Serikalini. Huu ni mgogoro mpya,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo
hilo jana alipokutana na watumishi wa wizara hiyo jana (Jumatatu, Julai 18,
2018) jijini Dar es Salaam, na kusisitiza kwamba hakuna sababu ya Serikali kuendelea
kuwa na watumishi wasiokuwa na uaminifu, uadilifu na uwajibikaji.
Alisema lengo la mkutano huo
ni kukutana na watumishi
kusikiliza changamoto zao, kukumbushana wajibu, pamoja na kutoa maagizo ili
yatekelezwe kwa utaratibu unaokubalika kisheria.
kusikiliza changamoto zao, kukumbushana wajibu, pamoja na kutoa maagizo ili
yatekelezwe kwa utaratibu unaokubalika kisheria.
Alisema mtumishi ambaye atabainika kuwa haitendei haki nafasi yake kwa
kutokutimiza majukumu ipasavyo hana sababu ya kuwepo kwa sababu serikali
inapoteza fedha nyingi kuwalipa watu wasio na tija.
Waziri Mkuu alisema sababu inayoikosesha Serikali mapato ni
uwepo wa watumishi wasio waadilifu kwenye ofisi za Serikali ikiwemo Wizara
ya Maliasili na Utalii hivyo kuna umuhimu wa kuzisafisha.
Alisema kuna uvunaji mkubwa wa misitu kuliko upandaji huku asilimia 50 ya mapato yatokanayo na uvunaji huo yanapotea na kuisababishia Serikali hasara ambapo alihoji sababu ya wizara kushindwa kusimamia jambo hilo.
Katika hatua nyingine; Waziri Mkuu aliitaka wizara hiyo kupunguza idadi ya vizuizi vya ukaguzi wa mazao ya
misitu kwenye barababara mbalimbali baada ya kukosa tija kutokana na upotevu wa misitu unaotokea kila siku.
Alitoa mfano wa barabara ya kwenda mikoa ya kusini kuanzia Dar es Salaam
ambapo alisema ina vizuizi visivyopungua sita na kila kizuizi kinatumika kwa ajili ya kukagua mazao ya misitu na maliasili inayotoka kuvunwa.
“Vizuizi vya katikati ya safari havina umuhimu na badala yake kuwe
na vizuizi mwanzo na mwisho ili rasilimali zingine zitumike kuongeza nguvu
na umakini wa ukaguzi kwenye vituo vichache vitakavyosalia,”.
“Kwa mfano ukitokea Ikwiriri kuja Dar, kuna vituo vya ukaguzi wa maliasili
visivyopungua sita, kuna Ikwiriri, Kibiti, Jaribu Mpakani,Mkuranga, Vikindu kote huku
wanakagua lakini linapofika kituo cha mwisho cha Mbagala linakutwa na makosa kwenye mzigo kwanini’’?
“Yule mkaguzi wa kwanza alifanya kazi gani? Kuna tatizo la uadilifu na
ninyi ni mashahidi, sasa naagiza ongezeni nguvu kwenye vituo vikuu vya
ukaguzi yaani mwanzo na mwisho,” alisema.
Aidha alisema ni muhimu kukawa na mabadiliko kwenye mfumo wa mauzo ya
misitu kutoka wa sasa (kuuza kwa eneo) na kuhamia kwenye mfumo wa mnada
ambao utaongeza mapato ya Taifa na utaweka uwazi.
Pia aliwataka watumie mashine za malipo za kielektroniki (EFD),wanapofanya mauzo ya mazao ya misitu ili
kuepusha matumizi ya daftari na risiti bandia ambazo hazitambuliwi na
wizara.
MAJALIWA: BARA LA AFRIKA BADO LINAKABILIWA NA CHANGAMOTO YA UPATIKANAJI WA MAJI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Bara la Afrika bado linakabiliwa na changamoto ya upatikanaji wa maji
safi na salama hasa vijijini kwa sababu nchi zake bado hazijamudu kuunganisha
huduma hiyo katika maeneo hayo.
Kufuatia hali hiyo, Waziri
Mkuu amewataka wataalamu wa masuala ya maji watafute njia sahihi itakayowezesha
kutatua tatizo hilo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji vilivyoko.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo
jana (Jumatatu, Julai 18, 2016) katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha
Julius Nyerere jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa 10 wa
Baraza la Mawaziri wa Maji wa Afrika (AMCOW) ambao unaokwenda sambamba na
maadhimisho ya Wiki ya Maji Afrika.
“Tunategemea baada ya
kumazika kwa mkutano huu wataalamu wetu wataondoka na maazimio mazuri ya
kumaliza tatizo la maji katika Bara letu kwa kutumia mito na maziwa ili
kufikisha maji kwa wananchi,” alisema.
Akizungumzia kwa upande wa Tanzania
alisema, suala la maji limepewa
kipaumbele hata katika bajeti ya mwaka huu na kwamba Serikali itahakikisha maji
yanapatikana katika maeneo yote ili kutimiza sera yake ya kila mwananchi kupata
maji umbali usiozidi mita 400.
Kwa upande wake Rais Mstaafu
wa Kenya Mwai Kibaki ambaye ni Mjumbe Maalumu wa UNESCO kwa ajili ya masuala ya
maji Barani Afrika alisema maji ni muhimu kwa maendeleo ya uchumi, hivyo wataalamu
wanatakiwa kuhakikisha huduma hiyo inapatika katika maeneo yote.
Mkutano huo wa siku tano unahudhuriwa Mawaziri wa Maji
kutoka nchi 45 za Afrika na unaongozwa na Waziri wa Maji na Mazingira wa
Senegal Amadou Mansour Faye ambaye ni Rais wa AMCOW.
(mwisho)
NSSF YACHANGIA MILIONI 50 HARAMBEE YA UJENZI MPYA WA LINDI SEKONDARI
Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Jamii NSSF Makao Makuu
ikishirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Lindi Imechanga Jumla ya Shilingi Milioni 50
Kwa Ajili ya Kuchangia Harambee ya Kusaidia Ujenzi wa Shule ya Sekondari ya
Lindi Iliyoungua Moto Wiki Iliyopita
Kwa Kutambua Umuhimu wa Elimu kwa Watoto Shirika Hilo Kupitia Mkurugenzi Mkuu
Wake ,Aliewakilishwa na Meneja wa Mkoa Bi Nour Aziz Limetoa ahadi hiyo kwa
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Majaliwa Kasim Majaliwa
Alieongoza Harambee Hiyo Ambayo Ilihudhuriwa na Wadau Mbali mbali Akiwemo Mke
wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Mama Salma Kikwete
Katika Harambee Hiyo Jumla ya Shilingi Milioni 80 Taslimu
zilichangwa Huku Ahadi na Vifaa vya Ujenzi zikifikia Shilingi Milioni 640
Ambapo Katika Ujenzi Mpya Waziri Mkuu Ameagiza Kujengwa Jengo la Ghorofa
litakalokuwa na Ofisi na Madarasa
Katika Tukio Hilo la Moto,Jumla Ya Madarasa 9 na viti na
Meza zaidi ya 300,Ofisi 4 na Vyoo Matundu 24 Viliteketea na Moto Uliotokana na hitilafu ya
Umeme
MAJALIWA: MARUFUKU WANAFUNZI KUTUMIA VIBERITI, MISHUMAA MABWENINI
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amepiga marufuku matumizi ya viberiti, mishumaa na hita za kuchemshia maji kwa
wanafunzi wa bweni ili kuepusha majanga ya moto na atakayekutwa atachukuliwa
hatua kali.
“Kuna tabia ya baadhi ya
wanafunzi hasa wa masomo ya fizikia kutengeneza vifaa vya kienyeji vya
kuchemsha maji mabwenini jambo hili ni la hatari kwani linaweza kusababisha
ajali ya moto, hivyo ni marukufu kwa mwanafunzi kutumia vifaa hivyo,” alisema.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Julai 17, 2016) katika
harambee ya kuchangisha fedha za ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari Lindi yaliyoungua
moto usiku wa kuamkia Julai 10 mwaka
huu.
Katika ajali hiyo shule imeathirika
kwa asilimia 34 ambapo vyumba tisa vya madarasa, jengo lenye matundu 26 ya vyoo
na jengo la maabara ya kemia na fizikia yameungua na kusababishia hasara ya sh.
milioni 682.78.
Waziri Mkuu amesema kwa
namna ambavyo majengo hayo yameungua ni vema yakavunjwa na kujengwa upya ambapo
aliwataka kutumia nafasi hiyo kwa kujenga jengo la ghorofa ili kutumia eneo
dogo kwa kujenga madarasa mengi.
Pia alimuagiza Mkuu wa mkoa
wa Lindi, Godfrey Zambi kuhakikisha fedha zitakazopatikana katika harambee hiyo
zinatumika kama ilivyokusudiwa.
Harambee ilihudhuriwa na mke
wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa, mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne, mama Salma
Kikwete, mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego pamoja na wadau wa maendeleo na
wanafunzi waliosoma shule hiyo akiwemo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,
Mhandisi Ramo Makani.
Katika
hatua nyingine Waziri Mkuu amezitaka taasisi mbalimbali
nchini kufunga vifaa vya kuzimia moto katika majengo yao kwa ajili ya kuvitumia
pindi ajali za moto zinapotokea.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
Tuesday, March 08, 2016
WAZIRI MKUU: RUSHWA YAPOTEZA DOLA BILIONI 150 AFRIKA
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema tatizo
la rushwa barani Afrika limesababisha bara hilo lipoteze dola za Marekani
bilioni 150 kila mwaka.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne,
Machi 8, 2016) wakati akihutubia wajumbe wa mkutano wa tano wa Bunge la Afrika
Mashariki (EALA) linaloendesha vikao vyake jijini Dar es Salaam. Mkutano huo
ulioanza Machi 6, utamalizika Machi 18, mwaka huu.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Dk.
John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu alisema rushwa imechangia kwa kiasi kikubwa
kurudisha nyuma maendeleo ya Jumuiya hiyo. "Rushwa yaweza kuwa kwa njia
kuhonga fedha, kupata fedha kwa kula njama, kujipatia fedha kwa njia za
udanganyifu, ama kwa njia za vitisho," alisema.
"Kwa mujibu wa taarifa ya Umoja
wa Afrika (AU), rushwa na urasimu vimeainishwa kuwa ni vikwazo vikubwa vinavyochangia
kuchelewesha ufanyaji wa biashara kwenye mipaka ya nchi za Jumuiya yetu,"
alisema.
Amesema sekta binafsi inachukuliwa
kama injini ya maendeleo na ukuaji wa uchumi na akatumia fursa hiyo kuipongeza
jumuiya ya wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kwa kuandaa kanuni za kiutendaji
ambazo zimelenga kuhamasisha uadilifu
kwenye ufanyaji biashara unaozingatia haki za binadamu, sheria za kazi,
utunzaji mazingira na vita dhidi ya rushwa.
Akizungumzia kuhusu uondoaji wa
vikwazo visivyohusisha kodi (non-tariff barriers) kama njia mojawapo ya
kuimarisha biashara kwenye jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema kwa upande wa
Tanzania, vizuizi vya barabarani kwenye barabara kuu ya Kaskazini vimepunguzwa kutoka
50 hadi vitano.
Alivitaja vizuizi vitano vilivyobakia
kuwa ni vile vilivyopo kwenye mizni ya Mikese (Morogoro), Nala (Dodoma), Njuki
(Singida), Mwendakulima (Shinyanga) na Nyakahura (Kagera).
"Sheria ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki ya uondoaji wa vikwazo visivyohusisha kodi ilipitishwa Machi 2015 na
sasa hivi inaendelea kusainiwa na Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Pamoja na mambo mengie, nia ya sheria hii ni kuondoa vikwazo vinavyosababisha
uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi, kurahisisha
sheria za biashara ndani ya Jumuiya yetu," alisema.
Akizungumzia kuhusu miradi ya
uwekezaji ya Jumuiya hiyo, Waziri Mkuu alisema miradi ya ujenzi wa barabara
inahitaji kiasi cha dola za marekani bilioni 20; ukarabati na upanuzi wa njia
za reli unahitaji dola za marekani bilioni 30; uendeshaji wa mashirika ya ndege
na viwanja vya ndege unahitaji dola za marekani bilioni 15; uendelezaji bandari
na usafiri wa majini unahitaji dola za marekani bilioni 10; utekelezaji wa
miundombinu ya nishati inahitaji dola bilioni 5 ambavyo kwa pamoja vinahitaji
dola marekani bilioni 80.
Alisema kuwepo kwa shughuli
mbalimbali za kiuchumi ndani ya jumuiya hiyo, kunaifanya Jumuiya ya Afrika
Mashariki kuhesabika kuwa ni jumuiya yenye nguvu kubwa ya kiuchumi barani
Afrika.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P. 3021,
11410 DAR ES SALAAM.
JUMANNE, MACHI 8, 2016.

Subscribe to:
Posts (Atom)